Watu wengi wa Japan wanachukia watalii

Watu wengi wa Japan wanachukia watalii

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,897
Reaction score
11,793
960px-Skyscrapers_of_Shinjuku_2009_January.jpg

Tokyo Japan


Wengi wetu tunawachukulia Wazungu kama watu wenye ustaarabu lakini sio kweli kama tunavyodhani.
Japan ina watu waliostaarabika kuliko wazungu na kwa mtu yoyote anayeijua Japan anaweza kunielewa.
1_Osaka.jpg

Osaka, Japan


Wajapan wanazingatia usafi, ukimya, ustaarabu na wengi wao hujali mambo yao hata treni za Japan huwa zipo kimya sana.
Japan hupokea takribani watalii milioni 25 hadi 35 kwa mwaka. Siku hizo watalii wamejaa na kuwa kero Japan huku wengi wao wakiwa ni watalii kutoka nchi za West, yani Nchi za Magharibi (including USA)

Siku za usoni kumekuwa na video nyingi za influencers jinsi walivyokuwa kero Japan kwa tabia zao zisizokubalika Japan

Kwa mfano angalia hii video, huyu dogo kutoka Ujerumani anazunguka nchi mbalimbali na spika yake then anaanza kupiga mziki kwenye mitaa. Kaenda pia kufanya hivi kwenye treni ya Japan ambapo watu wamezoea ukimya. Watu hawamwambii kitu ila kwenye sura zao unaweza kuona wanaboeka hadi mtu mmoja akaamua kuizima spika yake

Siku hizi watu wengi wamekuwa kero huko Japan. Wanaingia wanaanza kucheza mziki kwenye treni, wanapiga picha watu bila ridhaa yao, wanabembea na kufanya utoto kwenye maeneo ya kidini ya Kijapani ambayo Wajapan wanayaheshimu, wanajirekodi wanafanya Yoga kwenye ma temple ya kijapani yanayoheshimiwa na wana act kama vile wako nchini kwao bila kujali utamaduni wa Wajapani

Ukiingia mtandaoni utakuta video nyingi sana kuhusu namna ambavyo watalii wamekuwa kero Japan. Watu wengi wanapenda Japan kupitia utamaduni wao kama vile manga, Anime nk na kila mtu akiangalia Anime anatamani kutembelea Japan. Sio jambo baya lakini ni muhimi kuheshimu tamaduni za watu unapoenda kuwatembelea. Uafrika wako uache huku, ukienda kule ishi Kijapani. Na nina uhakika Waafrika wakifika Japan wanakuwa wastaarabu
Shida ni hawa Westerners, wanajiona kwamba wao ni VIP eti kisa tu wamelipa maelfu ya dollar kwenda Japan kwa hiyo wanajihisi Japan yote ni yao na wanaweza kufanya chochote for the sake of Content creation

Hii video ya mwisho inaonesha baadhi ya watalii wanaojiita Content creators wanavyoleta kero Wajapani

View: https://youtu.be/BR7B0Pjh3lE?si=mlkrcqWN_UH-2x59

Mwisho wa siku, tujifunze kuwa wastaarabu na watulivu kwenye nchi za watu. Sio kila sehemu unafanya unavyojisikia
Japan is not AMERICA. Respect the culture
 
Acha tokyo, acha Osaka , huko venice wao ni kwamba hawataki watalii zaidi, wamekuwa wengi hadi kero.
 
Zama hizi za uinfluencer na social media zimezaa watalii wapumbavu sana. Kuna yule John Somali. Amekera dunia nzima. Fikiria mtu anaikera dunia yote!
 
Zama hizi za uinfluencer na social media zimezaa watalii wapumbavu sana. Kuna yule John Somali. Amekera dunia nzima. Fikiria mtu anaikera dunia yote!
Umeona. Sasahivi kila mtu anaandaa content za kipuuzi ili apate likes na followers bila kujali hata impact yake kwenye jamii
 
Japs aka Kamikaze, ilikuwa moja ya jamii ya watu wakorofi sana.

Tehrani.
 
Inasikitisha sana niliona video moja mwanamke wa kijapani kajivalia zake nguo za kitamaduni anakatiza mitaani ghafla mtalii mmoja wa kike akaanza kumkimbiza ampige picha na video wanati mjapani hataki masuala hayo
 
japan ndio jamii pekee nyeupe ambayo ustaarabu ni tabia,haitokani na imani,mwendeleo wala elimu waliyo nayo.

huko hata tendo la ndoa huhesabika ni kwa ajili ya lengo maalum(uzazi)sio starehe.ni jambo la kawaida kukuta binti wa miaka 30 hajui kama kuna kupasuka.

na kwa tabia kama hizi za kutopenda ngono ndio sababu wanakaa umri mrefu sana,japan inaongoza kwa wazee,lakini ina tishio la upungufu wa watu maana watu hawajamiiani kuzaa.
 
Back
Top Bottom