Watu wazima wasiojua kusoma kwa ufasaha ni wengi sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,725
Kama upo humu JF au umefika chuo kikuu unaweza usione hili jambo sababu ya mazingira yako. Pia kama upo kazini unaweza hisi kila mtu anajua kusoma na kusoma kwa ufasaha. Ila ukija mtaani hili ni tatizo kubwa sana.

Kuna watu wamemaliza darasa la saba na hawajui kusoma, wasioweza kusoma kwa ufasaha ndiyo wengi ajabu. Kuna uwezekano kuwa nusu au zaidi ya raia wa nchi hii hawajui kusoma au hawawezi kusoma kwa ufasaha(wanasoma kama mtu wa darasa la kwanza au pili). Siku za karibuni nimekutana na watu wengi sana wasiojua kusoma na wanaosoma kwa taabu. Suala hili limenihuzunisha sana.

Umekutana na watu wa aina hii, nini kifanyike kuondoa aibu hii?
 
Hapo kwenye nusu au zaidi ndo inaonekana na wewe ni wale wale unavo sema nusu au zaid unamaanisha

Katika watu kumi watano hawajui kusoma au katika watu mia MOJA 50 hawajui kusoma au? Rudia utafiti wako
 
Mi nadhani utakuwa umekutana na wale wenye macho mabovu bilashaka
 
Back
Top Bottom