Watu watatu akiwemo muhitimu wa MUHAS wafariki katika ajali

Watu watatu akiwemo muhitimu wa MUHAS wafariki katika ajali

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Watu watatu akiwemo muhitimu wa udaktari chuo kikuu cha Muhimbili tawi la Tanga wamefariki na wengine watatu wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Ajali hii ni baada ya gari aina ya Noah waliyokuwa wakisafiria kutoka Dar-es-Salaam kwenda katika harusi mkoani tabora kupinduka na kubingirika mara tatu katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Singida.


========

Watu watatu akiwemo muhitimu wa udaktari chuo kikuu cha Muhimbili tawi la Tanga wamefariki na wengine watatu wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida , baada ya gari aina ya Noha waliyokuwa wakisafiria kutoka Dar-es-Salaam kwenda katika harusi mkoani tabora kupinduka na kubingirika mara tatu katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Singida.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoani Singida SSP Mayala Towo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo inasadikiwa kusababishwa na mwendo kasi wa gari aina ya noha namba T 878 CZY na dereva kushindwa kulimudu na kupinduka.

Kwa upande wao majeruhi ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida wamesema pamoja na dereva wao alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi ,lakini chanzo kilichosababisha ajali ni kupigwa na mwanga wa taa kali wakati wakipishana na lori na kusababisha kuacha njia na kupinduka.

ITV/Radio One ilipotaka kupata taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa mkoa wa Singida kuhusu majeruhi ambao wanapatiwa matibabu na vifo vilivyo tokea mganga mkuu wa mkoa Dr.John Mwombeki alitoa ruhusa ya kuwahoji majeruhi ,lakini hakuwa tari kuelezea mpaka kibali kitoke kwa katibu tawala wa mkoa ,na alipopigiwa simu katibu tawala wa mkoa wa singida Dr.Angelina Lutambi ili kutoa ruhusa simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.


Chanzo: ITV
 
Noah nadhani ni magari yanayoongoza kwa ajali hapa nchin Tanzania... Mtu uanpofikiria kununua Noah, fikiria mara mbili mbili... Walale pema peponi marehemu wetu...
 
Sad... Let's their souls rest where they belong
 
Noah nadhani ni magari yanayoongoza kwa ajali hapa nchin Tanzania... Mtu uanpofikiria kununua Noah, fikiria mara mbili mbili... Walale pema peponi marehemu wetu...

Noah haina shida ni ni sisi matumizi yetu, tunatumia vyombo vya moto kama ametengeneza shangazi yetu.
 
Back
Top Bottom