Watu wasiojulikana

Watu wasiojulikana

Forgo

Member
Joined
Apr 7, 2016
Posts
27
Reaction score
60
1: Walimuuwa Alphonce Mawazo (Chadema) kwa mapanga mchana kweupe.

2: Walimteka mwanamuziki Roma mkatoliki anayefanya harakati za kuikosoa serikali kupitia nyimbo zake na kumtesa kwa siku kadhaa halmanusra kumuuwa.

3: Walimzonga Nape Nnauye alipotofautiana na Serikali kuu na mmoja wao akaitoa bastora na kutaka kumshuti kichwani.

4: Huuwa watu na kuwafunga mikono na miguu na kisha kuwaweka ndani ya sandarusi na kuwatupilia mtoni au baharini.

5: Wamempiga risasi Mhe Lissu (Mbunge Chadema) na sasa yupo anapigania uhai wake.

6: Walivamia Clouds media wakiwa na mitutu ya bunduki wakiongozwa na Daudi Bashite.

7: Walimtowesha Benard Focus Saanane na mpaka sasa nchi nzima hatujui yu hai au wameshamuuwa.

»Kwanini Tanzania? (Sababu wenye akili wanaamua kuachana na siasa na wapumbavu ndio wanapewa madaraka).

»Kwanini wakati huu wa utawala wa Rais Magufuli? (Sababu hakushinda, alipitishwa kwa ubovu wa KATIBA tuliyonayo na ameonja utamu wa kuwa Rais na Amri jeshi mkuu na sasa anataka kutawala mpaka umauti utakapomfika).

»Kwanini ni wale tu wanaoipinga na kuikosoa serikali hii ya Magufuli? (Sababu hawa ndio watamkwamisha katika jitihada zake zakubakia madarakani milele).

Kwa akili zakipuuzi bado kuna mtu ataendelea kutowajua watu wasiojulikana na kuwaita ni watu wasiojulikana.

Tumezoeshwa ujinga na ujinga ndiyo jadi yetu.

#Lissu atapona kwa uweza wa Mungu na KATIBA kamwe haitobadilika @Mzinza_muuwaji_unayejulikana

Pia soma Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana


 
watu wasiojulikana waachieni wasiojulikana
 
Mbona "smoking gun" iko ndani ya dema yenyewe,au hamuioni.
 
Ni kizaazaa hao watu hawajulikani hadi leo

Get well soon Comrade Lissu
 
Back
Top Bottom