Watu wasiojulikana wavamia na kuchoma moto ofisi ya mtendaji mtaa wa Msewe

Watu wasiojulikana wavamia na kuchoma moto ofisi ya mtendaji mtaa wa Msewe

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
MKuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange amemuagiza Mkuu wa Polisi, Wilaya ya Kipolisi Kimara/Ubungo kuwatafuta na kuwakamata Watu wote waliovamia na kuchoma moto Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Msewe, na kuteketeza nyaraka na samano zote za ofisi hiyo.

Tukio hilo la kuvamia na kuchoma moto ofisi hiyo limetokea majira ya saa nne na nusu usiku wa April 25, 2025 ambapo nyaraka na samani zote zikiwemo viti na meza zimeteketea.

Baadhi ya mashuhuda wameeleza kuwa walishuhudia moto ukiwaka katika ofisi hiyo na hivyo kuanza juhudi za kuokoa samani na kuzima moto na kwa mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo Bi. Elizabeth Erick amesema Wahalifu hao kabla ya kuchoma moto jengo hilo waliiba meza na viti vipya vyenye thamani ya shilingi laki 4 na nusu.

Kufuatia tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongonzwa na Mkuu wa Wilaya ilifika na kujionea madhara yaliyotokea, ambapo amesema kilichofanyika ni uvunjifu wa amani sambamba na kulitaka Jeshi la Polisi kuwasaka Wahusika, akiongea baada ya kupokea maelekezo ya Kamati ya ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Kaimu Mkurugenzi Kissa Mbilla amewahakikishia Wananchi kuwa ndani ya siku saba ofisi hiyo itakarabatiwa na kurejesha huduma za kijamii kama zilivyokuwa awali.
 
Back
Top Bottom