Watu wasiojulikana wamvamia na kumkata mapanga dereva wa Mbunge wa Tarime, John Heche

Dereva wa mbunge, John Heche aliyejulikana kwa jina la Suez D Maradufu, amejeruhiwa na watu wasiojulikana jana kwa shoka. Dereva huyo alikuwa akielekea kwa mbunge, John Heche kwa ajili ya maandalizi ya kwenda Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu ambaye amelazwa Nairobi baada ya kushambuliwa na wanaharamu wanaodaiwa kutokufahamika.

Chanzo: Mwananchi.co.tz
Dereva wa mbunge ajeruhiwa kwa shoka

Naanza kuona the reincarnation of Ku Klux Klan, nchini Tanzania.
 
Jana majira ya saa mbili usiku dereva wa mbunge Mh. John Heche anayejulikana kwa jina la SUEZ DANIEL MARADUFU alivamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kwa kukatwa katwa na mapanga kichwani na hali yake si nzuri, anaendelea na matibabu kwenye hospitali ya Bomani Tarime.

Ofisi ya Mbunge
jimbo la Tarime Vijijini
15/9/2019
Nan wabunge wetu waache kutembea na wake za watu kwa nguvu wakipigwa wanasingizia siasa Kumbe ni ushenzi wao mtaani
 
Hivyo wanaishi pia nje ya siasa awamu hii tuu
Awamu zilizopita hawakuwa na maisha binafsi
Ficha aibu
Kwa sababu awamu iliyopita wengi wenu mliokuwa mnatumia vyeti feki mlikuwa mnakamua vya kutosha. Na Mafisadi walikuwa wanafanya yao. Bila kusahau wauza ngada. Awamu hii vyuma vimekaza. Mnatoa series tu kila kukicha.
 
JF Kwenu,

Katika muendelezo wa visa vya watu wasiojulikana:
Dereva wa mbunge wa Tarime Mh. John Heche, amevamiwa na kupigwa mapanga usiku wa kuamkia leo.
Dereva huyo anaejulikana kama Suez Daniel Maradufu, amelazwa katika hospitali ya Bomani akipatiwa matibabu.

Mh. Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kupitia kwa katibu wake, Mrimi Zablon.

Kamanda wa polisi kanda ya Tarime-Rorya,Henry Mwaibambe alipotafutwa kuthibitisha tukio hilo alisema yuko kikaoni, atatoa taarifa baadaye.
 
Watu wasiojulikana wanaopata maelekezo toka juu
 
Badala ya kumwaga fedha mitaani hali ngumu nyie mnamwaga damu aya endeleeni tuone damu ya nani itasalia
 
Back
Top Bottom