Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Kumekuwa na habari nyingi za waganga njaa na wanufaika wa utawala wa mwendazake kwamba eti anachafuliwa Ili kufuta legacy yake.
Binafsi nimekuwa mfuatiliaji wa Ripoti za CAG yangu mwendazake ashike madaraka na hakuna hata siku moja Ripoti iliwahi kuwa nzuri chini ya utawala wake.
Miaka yote kumekuwa na uozo huo huo na mbaya zaidi uozo umekuwa ukiongezeka na hakuna hatua zozote ambazo serikali ya mwendazake ilichukua kubadili mambo.
Tofauti iliyopo sasa ni kwamba CAG ametakiwa kutamka yote sio sawa na kipindi kile ambapo alichagua ya kuongea.
Nadhani mnakumbuka kashfa ya 1.5trilioni na uozo wa fedha za matibabu ya spika na matumizi mabaya ya wizara ya maliasili na taasisi zake kujilipa posho.
Nadhani hata Ripoti ya sasa ni muendelezo wa uozo ule ule wa serikali ya mwendazake na bado CAG amepitia juu juu tuu kwenye masuala ya ndege na miradi mikubwa.
Kwa maana hiyo waimba mapambio na wanufaika wa mwendazake watulie maana waliwaziba watu midomo kwa mkono wa chuma huku wakiimba propaganda ya uzalendo na kutetea wanyonge huku wakijinufaisha wao na genge lao.
Muacheni mama asimamie uhuru wa kujieleza Ili kukomesha tabia za wizi na kuwaumbua wezi.