Watu Wanne watiwa mbaroni kwa tuhuma za kutumia jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutapeli

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo jana kujibu mashtaka 12 yanayowakabili, likiwamo la kughushi barua na kuziwasilisha katika vituo vya mafuta wakirubuni watumiwe kiasi cha fedha ili waweze kupata punguzo la kodi.

Washtakiwa hao ni mwanafunzi, Issa Mohamed Awadhi (27)
maarufu kama Charles Robert au Mwamunyange, mkazi wa Ilala, ambaye hakuwapo mahakamani hapo kutokana na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua.

Wengine ni Hamisi Tembo(37) mkazi wa Ilala, mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado(32), mkazi wa Mbagala Kuu na Wakati Mungi (51) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo Makangarawe.

Washtakiwa walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kukosa dhamana. Kesi itaendelea Aprili 11.
 
Duh! Sikutegemea kama Hamis Tembo kwenye michezo hii, huyu jamaa ni mtangazaji wa Radio Imaan, labda awe ameacha kazi jana au juzi. Pia, ni msemaji wa taasisi moja ya Hijja, na ni swahiba mkubwa wa Ridhiwan JK.

Ova
 
Back
Top Bottom