Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Fikra hizi ndizo zinatufanya tuzidi kuwa masikini.
Umasikini upi wakati tutakuwa na treni ya umeme kwa umbali wa kilomita zaidi ya 1000 kitu ambacho hata Marekani hakipo.
 

Liangalie hili lipenda madaraka zaidi ya uhai za watu!

I couldnt careless mtawale mpaka lini au mlete maendrleo kiasi gani,jinsi mnaua na kuteka watu nimechukia kabisa!

Nimeona mnachofanya ni mavi kabisa,when you started killing innocent people!

Go to hell with huo upumbavu unaojifanya ni maendeleo which sio maendeleo to begin with!
 
Yeye pia ni kundi la wapigaji angependa maendeleo angeanza na utengenezaji wa chuma cha mchuchuma, liganga, na chuma cha pua songwe yeye ananunua chuma kutoka nje kama sio sababu ya dili ni nini huoni una mahindi ndani badala ya kusaga upate unga unakwenda dukani kununua unga huo ni wizi mkubwa
 
Kama unaongelea reli kuagizwa kutoka Japan, elewa kuwa Tanzania hakuna kiwanda cha kutengeneza machuma ya reli nzito zenye uwezo wa kubeba tani 35 hivyo ilibidi tuagize. Ila hiyo la mchuchuma na kiwira nadhani linafanyiwa kazi kwa sasa ili tuweze kufua vyuma vyetu hapo baadae.
 
Inaonekana wewe hauko nchini. Umeambiwa kuna watu wanabeza au kupinga maendeleo yanayofanywa na rais nawe umeamini. Umepewa list ya watu hao wanaopinga yale rais anafanya? Kama ndivyo iweke hapa.

Kinachopingwa si shughuli za maendeleo yanayofanywa bali namna yake ya ufanywaji wa shughuli hizo za maendeleo.

Kazi yoyote ikifanyika nje ya mipango ni takataka hata kama iwe nzuri namna gani. Ni kwasababu hiyo kanyima watumishi haki zao za kiutumishi kwa kisingizio cha miradi ya kimaendeleo. Mipango yake ilikuwa kunyima haki watu ndipo shughuli hizo za maendeleo zifanyike? Alishauriana na nani? Mtu unayefanya mambo bila kushauriana na wenzako wewe ni mtu?

Kila rais amefanya mazuri na mabaya wakati wa utawala wake hapa nchini. Lakini naomba uamini, huyu kawazidi wote katika mabaya. Siku akitoka madarakani ndipo utanielewa kwasababu utasikia atakavyopondwa tena na hao hao wanaomsifia leo.
 

Halafu katika hali ya kushangaza, hatujawahi kusikia akijipunguzia posho, marupurupu, mshahara wake na ule wa wasaidizi wake ili kuwaunga mkono hao anao wanyanyasa kila uchao kwa kigezo cha kujenga miundombinu na kununua ndege! Yeye anapenda kuishi maisha ya peponi, ila wengine tuishi maisha ya jehanamu!

Binafsi sikuwahi kuwaza kama mzee wa msoga angekua bora mara mia kwa wafanyakazi kuliko huyu!
Zaidi ya ubinafsi, chuki, roho mbaya ya kwa nini, roho ya kimaskini, ukatili, uonevu, nk hakuna dhamira nyingine unaweza kuifikiria kwa huyu kiumbe dhidi ya watumishi wa umma.
 
Hivi hii dhana ya Rais ni mtu mmoja imetoka wapi? Yeye anapewa taarifa na kushauriwa cha kufanya na kutoa maamuzi. Hivyo mambo ya watumishi kutopandishwa madaraja hilo ni suala la muda tuu ila kwa sasa cha muhimu ni kuwa na miundombinu ya uhakika.

Haiwezekani kukatika kwa umeme iwe jambo la kawaida, watoto wasihudhurie shule kwa kukosa ada. Inashangaza watu kuona sawa mtu akitaka kwenda Kasulu - Kigoma wakati wa masika haiwezekani kwakuwa barabara zinamatope. Yaani watu wanaona sawa kutumia masaa matatu kuvuka kivuko cha Busisi - Kigongo wakati unatakiwa kutumia dakika tatu tuu.

Kupanga ni kuchagua.
 
Mkuu, hawa wanaolialia humu jukwaani wengi wao ni wale waliotumbuliwa kwa namna moja au nyingine. Ni wahanga wa chekeche zito la awamu ya tano.

JPM anayatazama maslahi mapana ya Tanzania bila ya uoga, wanajaribu kumkwaza lakini wanaomuunga mkono ni wengi kuliko hawa wenye hasira.
 

Akili za wana ccm bhana! Kwa hiyo mtu anapodai haki yake basi huyo ametumbuliwa! Mjibu hoja; kwa nini yeye mwenyewe asiwe mfano wa kuigwa kwa kujipunguzia stahiki zake na zile za wasaidizi wake ili kujenga hiyo miundombinu?

Why watumishi wa umma tu wanyimwe haki zao? Kwa nini lisiwe zoezi la kitaifa? Mtu wa namna hii utamuita jina gani zaidi ya mbinafsi na mtu mwenye roho ya kwa nini? Hakuna anayepinga maendeleo! Lakini ni kwa nini uwaumize wachache? Mbona JK alijenga kila aina ya miundombinu lakini aliheshimu haki za wafanyakazi?
 
Mkuu haya yanayofanyika ni kwa nia njema inayolengwa kwa hao hao wafanyakazi.

Ni muhimu mtu aishi vizuri lakini kumbuka kuwa Tanzania haishii na uhai wako na wa kwangu na wa mwingine aliyehai leo hii.

Haya madaraja na ndege na miradi mingine mikubwa inamlenga mtanzania wa mwaka 2045- 50. Ndicho walichokifanya wazungu miaka mingi iliyopita, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayotumika hivi leo.

Tuvumilie machungu ya sasa, kinachofanyika kinatazama mbali zaidi, tujitahidi tuuepuke ubinafsi, maisha hayaishii kwa sisi wa sasa, wapo watanzania wa miaka 50 mpaka 100 ijayo.
 
Mbona tani za chakula ni nyingi lakini wakulima bado masikini wa kutupwa?
 
Count ya maendeleo ya taifa ni pamoja na usalama wa raia wake. Hili tumerudi nyuma miaka 50 +.
 

Mkuu mimi kinachoniuma ni kwa nini ameliangalia kundi moja tu la watumishi wa umma! na siyo yeye mwenyewe, bunge, wasaidizi wake, nk. Wakati wa JK, haya mambo yote yalifanyika kwa wakati mmoja. Madhara ya kutopandisha madaraja ni makubwa kupindukia!

Bora angeacha kuongeza mshahara, ila siyo daraja la mfanyakazi. Huku makazini kwa sasa ni kichekesho, mtumishi aliyeajiriwa mwaka 2013, 2014, na kuendelea; na huyu wa mwaka 2019, wote wako daraja moja! Hii haileti mantiki kabisa! Ni uonevu usio na kipimo.
 
Lumumba nyie walamba miguu muwe mnaelewa ,hakuna anayepinga maendeleo sawa watu wanapinga vitendo vya ushetani vya Jiwe ,pamoja na vipaumbele vya miradi eleweni nyie ma slow learner .
 
.Atakayebisha kuwa kiongozi hajaleta maendeleo nchini huyo ni muongo maana mwenye macho haambiwi tazama isipokuwa angeanza kutekeleza ujenzi wa reli standard gange limalizike ashike lingine .Kutekeleza miradi yote kwa pamoja kutawahumiza wananchi kwa kodi kuongezeka nakudumaa kwa umasikini.Halafu kiongozi wetu aruhusu ushirikishwaji wa wananchi wote kujenga nchi yao bila kuwa na ofu yeyote ..Uongozi wa demokrasia ndio utakayepandisha chati kiongozi wetu ngazi ya kitaifa na kimataifa .
 
Mkuu kwa mtazamo na uelewa wangu hivyo vyote ulivyovitaji si maendeleo ila matokeo ya maendeleo,hivyo vitu tunavijenga kwa kukopa pesa toka nje,lakini hao wanaotukopesha hivyo vitu wanavyotayari,je wao walikopa wapi?Jibu ni kwamba wao walitafuta maendeleo ya watu wao kwanza kwa maana ya kuhakikisha watu wao wanapata elimu bora,watu walipoendelea uwezo wao wa kulipa kodi ukaongezeka,serikali ikakusanya pesa ya kutosha ndo ikaanza kufanya hivyo unavyoita maendeleo, acha tujidanganye tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…