Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Akishafanya yote hayo nani atayatumia maana either watu tutakua hatuna nauli hata ya ku afford au wengi watakua washatangulia mbele ya haki kwa magonjwa ya moyo na saratan zilizosababishwa na ugumu na ukali wa awamu hii......

Ukitaka maendelea ya kweli lazima uangalie pia nabya raia mmoja mmoja
 
Maendeleo ni pamoja na kuteka watu?, kuua watu?, kutesa watu, kupiga risasi watu?, kunyanyasa watu?, kama hayo nayo ni maendeleo basi hatuyataki maendeleo ya namna hiyo
Uzuri ameandika ni maendeleo ya Magufuli..kama Nchi bado sana...hakuna cha maendeleo zaidi ya unafiki..[emoji41]
 
Kwako wewe kama ungepata nafasi ya kuongoza ungeanza na nini?
Kwani watu wanapopanda mabasi sasa wanapanda bure?
Sababu ya kutopandishwa madaraja mwenyewe alisema kwasasa tunajenga miundombinu, huu ni wakati wa kujifunga mikanda.
 

Hukuwepo wakati wa Nyerere mambo mengi yalikuwa yanafanywa kwa amri hujui tu, inawezekana ni kijana mdogo huelewi, ulizia watu au wazazi wako, kulikuwa na mambo mazito yalikuwa yanatekezwa leo isingewezekana kabisa, oparesheni vijiji iliacha watu na majunzi makubwa, vita vya kagera,watu binafsi walikuwa hawaruhusiwi kumiliki biashara, kununua Magari kwa vibali, vita vya uhujumu uchumi iliacha watu na majonzi makubwa, nadhani watu wengi umri mdogo, hawajui tulikotoka, hapakuwa na matusi kama kizazi hiki,
 
Chamoto,

..natofautiana na wewe kuhusu treni ya umeme kusafirisha wauza sangara.

..pia natofautiana na Naibu Waziri Mh.Mavunde aliyedai treni ya umeme itakuwa ikisafirisha wauza mchicha.

..Kama hayo ndiyo matarajio ya aina ya mizigo itakayokuwa ikisafirishwa na sgr basi taifa litaingia ktk hasara na mzigo mkubwa wa madeni.

..kuhusu kilimo umeeleza kuhusu kuongezeka kwa uzalishaji toka mwaka hadi mwaka.

..Sasa kuna kiwango cha ukuaji ktk sekta ya kilimo, nadhani ni asilimia 9 kila mwaka, ambacho wataalamu wa uchumi wanasema lazima tukifikie.

..Na ukuaji huo unapaswa uwe sustained kwa miaka kadhaa. If we do not reach that target wataalamu wanasema masikini hautakwisha hapa Tz.

..Nadhani unanielewa kwanini naona Jpm amepungukiwa ktk mbinu za kuikwamua nchi yetu toka ktk umasikini.
 
Nadhani wapingaji hawana tatizo na maendeleo, wana tatizo na anayeleta hayo maendeleo (labda hawampendi) maana barabara watazitumia, ndege watapanda na hawajagoma kuchangia kodi.
Swali sahihi linaweza kuwa ni kwanini wapingaji hamumpendi wakati anawaletea maendeleo?

Ni sawa na mwanamke anayezitaka pesa zako Ila wewe hakutaki, atakuponda tu ila ela atachukua.
 
Ndege na sgr ni hasara tu... Upotevu wa pesa...
Bora ata anepambania barabara pekee uku akihakikisha wakulima wanamazingira mazuri..


Utasafirisha nini?
 
Maendeleo ni pamoja na kuteka watu?, kuua watu?, kutesa watu, kupiga risasi watu?, kunyanyasa watu?, kama hayo nayo ni maendeleo basi hatuyataki maendeleo ya namna hiyo
Ili uendelee lazima utakutana na wapingaji na wasaliti na hukumu ya msaliti ni moja tu nayo ni kumwondoa duniani na kumpeleka kwa Mwenyezi Mungu ili akapata hukumu stahiki.
 
maendeleo ya magufuli? maendeleo ya nchi
 
hiy mwaka jana wakulima wa KOROSHO WALIPORWA KOROSHO ZAO
 
Ili uendelee lazima utakutana na wapingaji na wasaliti na hukumu ya msaliti ni moja tu nayo ni kumwondoa duniani na kumpeleka kwa Mwenyezi Mungu ili akapata hukumu stahiki.
unamkumbuka kijana wa MAKAMBO? RAISI ALIAMRISHA ASHIKISHWE ADABU/ APIGWE KISA KABEBA BANGO LENYE UJUMBE WA MAJI
 
Naona hukuelewa muktadha wa hayo maneno, haikumaanisha kuwa reli yenye axel load ya tani 35 itakuwa ikibeba mchicha bali abiria (wananchi wa kawaida), wafanyabiashara wadogo wadogo wanaweza beba michicha yao humo.

Hiyo ilikuwa kuonesha kuwa treni hiyo itafaidisha watu wote.
Ongezeko la mazao kwa mwaka huu lilikuwa ni 124%
..Nadhani unanielewa kwanini naona Jpm amepungukiwa ktk mbinu za kuikwamua nchi yetu toka ktk umasikini.
Kuna sekta nyingi ambazo serikali hii imeziimarisha ikiwemo madini, sasa hivi mapato yaliyokuwa yanapatikana kwa mwaka sasa yanapatikana kwa siku moja.

maendeleo ya magufuli? maendeleo ya nchi
Maenedeleo yaliyoletwa na Magufuli.
hiy
mwaka jana wakulima wa KOROSHO WALIPORWA KOROSHO ZAO
Wale waliostahili walilipwa.
 

Kama maendeleo ndio kitu pekee kinachofanya matawala aungwe mkono, kipi kilitufanya tuwaunge mkono waeusi wa Afrika kusini wakati wazungu waliweka maendeleo mara mia ya haya ya Magufuli?
 
Kama maendeleo ndio kitu pekee kinachofanya matawala aungwe mkono, kipi kilitufanya tuwaunge mkono waeusi wa Afrika kusini wakati wazungu waliweka maendeleo mara mia ya haya ya Magufuli?
Ni wapi nimesema maendeleo ndiyo kila kitu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…