Watu wanaojifanya wanadini wanakuwa na roho mbaya sana

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Binafsi sivuti sigara ya aina yoyote, sinywi pombe, siendi kumbi za starehe nk lakini katika kuishi kwenye mikusanyiko ya watu wengi nimegundua wale watu ambao hawajinasibishi na dini sana japo wanaamini katika Mungu wanakuaga watu fair sana.

Kama ni hostel unaweza kushare vitu vyao vingi tu na mambo mengi wanachukulia kawaida/ easy, ila waoe wa dini mmh! Yaani kila kitu wanachukulia serious halafu wana roho mbaya. Hawapendagi kushare vitu vyao kama chaja, pasi na vitu vingine. Wanajifanya wanajua mambo mengi, wanapenda visasi nk.

Siwasifii walevi, au sisemi watu wasiabudu Mungu, ila tu jamaa wasio hao wako flexible sana na ni rahisi zaidi kuishi na msela kuliko mchungaji au ustadhi, wengi wako fixed and closed in mind.
 
Respect people's opinions especially kw vile wanavyomiliki.They r free to decide whatever.

By the way u r not in position to decide how people should treat u.Ukiona hawako fare kaa nao mbali miliki na ww vitu vyako utakavyokuwa huru navyo kuamua chochite.

Usijitese sana mkuu ndio dunia ilivyo.
Muungwana hanuni kwa kuvimba mashavu bali moyoni
 
We umefanana na jamaa yangu sasahivi katoka kulalamika eti chumba alikokuwa anakaa na mshkaji wake kafukuzwa. Mwenye chumba eti anahama,nikamwambia tulia si kila mtu anapenda kuishi maisha ya kubanana. Huyu jamaa ni mtumishi,yuko chuo na hana mkopo
 
maisha yana kero zisizoisha.ukipangua hii kesho inakuja nyingine.

leo kakosa uvumilivu kwa mwana,sawa.
kesho anakuja kubanwa na kaka yake mkubwa.
 
Binafsi sivuti sigara ya aina yoyote, sinywi pombe, siendi kumbi za starehe nk lakini katika kuishi kwenye mikusanyiko ya watu wengi nimegundua wale watu ambao hawajinasibishi na dini sana japo wanaamini katika Mungu wanakuaga watu fair sana.

Kama ni hostel unaweza kushare vitu vyao vingi tu na mambo mengi wanachukulia kawaida/ easy, ila waoe wa dini mmh! Yaani kila kitu wanachukulia serious halafu wana roho mbaya. Hawapendagi kushare vitu vyao kama chaja, pasi na vitu vingine. Wanajifanya wanajua mambo mengi, wanapenda visasi nk.

Siwasifii walevi, au sisemi watu wasiabudu Mungu, ila tu jamaa wasio hao wako flexible sana na ni rahisi zaidi kuishi na msela kuliko mchungaji au ustadhi, wengi wako fixed and closed in mind.

Wavuta sigara ndiyo wanaongoza jwa kushirikiana duniani, mvutaji mmoja anaweza akamkuta mwenzake anavuta sigara akagonga vidole na kuchukua sigara anavuta mpaka anakata hamu yake anarudisha anaondoka bila salaam wala kuagana, lakini sisi wafia dini hatupeani hata kiberiti na runawaona wavuta sigara watu wa motoni siku ya mwisho.

Wanywa pombe hali kadhalika, zamani walipokezana buyu moja linazunguka midomo kumi bila kupukuta na kadri buyu lilivyozunguka toka mdomo mmoja hadi mwingine ndivyo utaamu wa pombe uliongezeka.

Vitabu vitakatifu vinahubiri upendo kwanza, na upendo huo tunauona kwa watumia sigara na pombe ya buyu. Je Mungu hawaoni hawa kama ni bora zaidi kwakuwa wanatimiza agizo lake la upendo?
 
Sipendi kushare vitu jamani aiseee. Mtu hadi nguo anataka kuazima,kiatu aazime,hereni,mkufu,saa aah bora kuitwa roho mbaya
Mambo ya kuazimana mpaka nguo tuseme vitu vya kuvaa mwilini hapana hata mie hilo katu sikubaliani, labda itokee emergency lakini eti kaamua tu ni mwazime nguo no
 
Kuazimana kupo lakini kuna watu huazima mpaka vitu hivyo kuonekana vyao, kwanini mtu usitumie ulivyo navyo, kuazima kusiwe kero kwa wenyewe mtu unaazima mpaka soksi?
 
Back
Top Bottom