Watu wamechoka na chaguo la Mungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu wamechoka na chaguo la Mungu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 19, 2008.

1. BAK

BAK JF-Expert Member

#1
Oct 19, 2008
Joined: Feb 11, 2007
Messages: 70,813
Likes Received: 83,204
Trophy Points: 280
Watu wamechoka na chaguo la Mungu?

Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KWA muda wa wiki moja sasa, Rais Jakaya Kikwete yupo mkoani Mbeya akiendelea na ziara yake ya siku 10, kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya mkoa huo. Pamoja na kukagua shughuli za maendeleo, rais pia anapata fursa ya kuzungumza na wananchi.

Katika kuzungumza huku, kwa kuwa hii ni mara yake ya kwanza kwenda Mbeya tangu achaguliwe kuwa Rais, ni dhahiri kuwa anatumia wasaa huo kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kumpa kura. Amekuwa akifanya hivi kila mkoa anaotembelea.

Pia, kwa upande mwingine, ratiba ya rais kuzungumza na wananchi, inatoa fursa ya aina yake kwa wananchi nao kuzungumza na rais. Bila ya shaka, katika mazungumzo yao, wananchi hao wamekuwa wakimsuhukuru rais kwa kuwatembelea. Baada ya hapo, hufuata mlolongo ya malalamiko yakionyesha kero na matatizo wanayokabiliana nayo.

Ni dhahiri kuwa kero za watu wa mkoa wa Mbeya ni nyingi sana kwa sababu zimerundikana kwa muda mrefu. Hii inatokana na Rais Kikwete, kuaharisha ziara ya kuutembelea mkoa huo. Kumekuwa na maneno mengi sana kutokana na hilo, ingawa kwa sasa, inaelekea kuwa linageuzwa kuwa suala la kisiasa zaidi.

Katika ziara hiyo ya mkoani Mbeya, Rais Kikwete, amekumbana na mkasa wa aina yake pale msafara wake uliporushiwa mawe na wananchi wa kijiji cha Kanga wilayani Chunya, baada ya wananchi kumsubiri siku nzima lakini alipopita hapo hakusimama kuwasalimia. Wananchi hawa walimsubiri kwa hamu kubwa rais wao, ili wamweleze yao ya moyoni, lakini aliwapita akiwaachia vumbi tu.

Bila ya shaka, subiri yao ilitokana na ratiba waliyopewa ikionyesha kuwa rais atasimama hapo na kuwasalimia. Ndiyo maana walijiandaa. Kama wangekuwa wameambiwa kuwa rais hatosimama hapo, sidhani kama wangejisumbua kukaa kumsubiri.

Kimsingi hatua hiyo ya wananchi kuurushia mawe msafara wa rais, ni jambo lisilokubalika katika jamii ya kistaarabu. Lakini pia ni jambo la hatari yenye kutia aibu kwa viongozi, akiwamo kiongozi mkuu wa nchi, ambaye kila kukicha amekuwa akihimiza uvumilivu, mshikamano na umoja baina ya Watanzania.

Jamii ya watu waliostaaribika hawapaswi kufanya kitendo kama hicho, bali hutumia njia za kistaarabu kufikisha ujumbe wao. Licha ya kuwa ni aibu yenye kusababisha hasara, vurugu kama hizo zinaweza kusababisha mtu kukamatwa, kushitakiwa na kufungwa jela kwa muda mrefu. Pia tabia hiyo inaweza kusababisha majeraha kwa watu wengine ambao hawahusiki kabisa na hasira za wananchi.

Wananchi walianza kwa kuwazomea mawaziri na watendaji Serikali waliokuwa wakitembea mikoani kutangaza uzuri wa bajeti mwaka jana. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kihistoria. Lakini mwitikio wa wananchi ulipaswa kuwa somo kwa viongozi hawa.

Baada ya matukio hayo, walipaswa kukaa na kujiuliza kulikoni wananchi ambao walikichagua chama chao kwa kura nyingi, wameanza kuzomea? Sijui kama hili lilifanyika.

Wananchi walikerwa na ziara hizo ambazo zilikuwa zikitumia mamilioni ya shilingi huku wao wakiogelea katika lindi la umasikini. Waliamini kuwa fedha zilizotumiwa na mawaziri kuzunguka mikoani, zingeweza kutumika kuboresha zahanati, kununua dawa, kujenga shule, barabara, huduma za maji na nyingine ambazo ni mbaya.

Hasira za wananchi hao zinaelekea kukua hivi sasa na hata kufikia kuonyesha chuki za wazi kwa kiongozi mkuu wa nchi ambaye wamethubutu kuurushia mawe msafara wake kwa kile kinachodaiwa kuwa rais hakusimama eneo lao ili wamweleze matatizo waliyo nayo.

Kitendo hicho kinaonyesha jinsi wananchi walivyokata tamaa ya maisha kiasi cha kuwa tayari kufanya vitendo vya hatari ambavyo wakati mwingine vinaweza kusababisha vifo au vilema vya maisha.

Kama askari waliokuwapo kwenye ziara hiyo wangeamua kuwafyatulia risasi wananchi hao kwa vyovyote hali ingekuwa mbaya zaidi na pengine tungeshuhudia vurugu tunazoziona kwenye vyombo vya habari zikitokea nchi nyingine mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika.

Dalili za hasira za wananchi na kuishiwa kwao uvumilivu zilionekana tangu mwanzo wa ziara hiyo pale wakazi wa Mwanjelwa, Mbeya walipousimamisha msafara kwa kulala barabarani. Hao walimtaka rais awafikishe mahakamani mafisadi walioiba fedha za EPA, wala rushwa na kutimiza ahadi zake za maisha bora ambayo sasa zinaonekana kutotekelezeka. Alipowajibu na wao kwa kuonyesha kutoridhishwa na majibu yake, inadaiwa kuwa walizomea.

Ni jambo lililo wazi kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ugumu wa maisha unavyozidi na hata wananchi waliokuwa wakimudu kula milo mitatu kwa siku hivi sasa wanapata mlo mmoja.

Wakati wananchi hao wakipata mlo mmoja kwa siku, kila kukicha, watendaji wa Serikali wamekuwa wabunifu kutafuta magari ya kifahari na samani na kununua kwa bei ghali bila kujali kilio cha maisha magumu ya wananchi.

Hivi sasa Serikali imenunua magari mapya aina ya Toyota Land Cruizer V8 kwa ajili ya mawaziri wake, ambayo bei yake kila moja haipungui sh milioni 100.

Kila kukicha nchi imekuwa na migomo ya wafanyakazi isiyomalizika, huku juhudi za kuitatua migomo hiyo zikionekana kuwa ni dhaifu na hata watendaji wa Serikali nao wanaelekea kutokuwa na mbinu mpya za kutatua matatizo. Sasa wamegeuka kuitegemea mahakama!

Kwa ujumla, nchi inaelekea kubaya na ni vema Rais Jakaya Kikwete, akasoma alama za nyakati, na kuchukua hatua mufaka ili kukomesha hali hii. Kama asipoangalia, hali itegeuka kuwa mbaya zaidi na akichelewa kuchukua hatua, itafika mahali atashindwa kabisa kuwa na udhibiti wa hali ya mambo.

Watanzania ni mashahidi wazuri wa ahadi alizozitoa rais Jakaya Kikwete. Mojawapo ikiwa ni ile ya kuzalisha ajira milioni moja, jambo ambalo kwa hivi sasa linaonekena kuwa gumu kwani watu wengi hivi sasa wanapoteza ajira zao.

Leo hii Rais kikwete anapouambia umma kuwa ameongeza ajira kwa Watanzania kuanzia kwa wafanyakazi wa ndani, wafanya usafi bustanini, wachunga ng'ombe na wengineo ni jambo la kushangaza sana.

Ajira wanazoitaka Watanzania si hizo alizozitaja, bali ni zile zinatotambulika na zenye mchango mkubwa kwa taifa kwa maana ya kuingiza mapato yanayotokana na kodi za mishahara ya wafanyakazi pamoja na kuwa na pensheni mtu akifukuzwa au kustaafu kazi.

Ajira hizo anazojisifu nazo rais Kikwete zilikuwapo tangu zamani, hivyo hakuwa na haja ya kujisifia kuwa ameongeza ajira kwa Watanzania.

Leo hii Serikali imekuwa ikiimba wimbo wa uchumi kupanda, lakini ukiangalia maisha ya mwananchi wa kawaida yanazidi kwenda mrama siku hadi siku. Mambo kama haya yanawafanya wananchi wajuione kama wanahadaiwa.

Moja kati ya dai walilolitoa wananchi wa Mbeya walipomzuia Rais Jakaya Kikwete ni kuhitaji maji ambayo aliwaahidi alipokuwa akiwaomba kura zao lakini mpaka sasa bado hawajayaona.

Kwa hali ilivyo hivi sasa, inaelekea rais Kikwete ameelemewa na mambo mengi na anashindwa kuzitekeleza ahadi zake alizozitoa alipokuwa akipita kuwaomba wananchi ridhaa zao za kumchagua kukalia kiti cha urais kwa tiketi ya CCM.

Wananchi waliamini ugumu wa maisha utatoweka pindi wakimpa kura Rais Kikwete, ndiyo hao hao waliokata tamaa ya maisha na kuamua kumrushia mawe au kuwazomea watendaji wake.

Inasikitisha kuona nchi ya Tanzania yenye rasilimali za kila aina ikiendelea kuwa maskini kwa sababu ya rasilimali zake kubinafsishwa kwa wawekezaji kwa bei za kutupa.

Kurushiriwa mawe huko ni dalili mbaya zaidi kwani inaonyesha kuwa kama wananchi hao wangekuwa na silaha za kisasa basi mambo yangekuwa mengine.

2. M

Mwikimbi JF-Expert Member

#2
Oct 19, 2008
Joined: Mar 8, 2008
Messages: 1,745
Likes Received: 109
Trophy Points: 160
Mwinjilisti: Mbeya kulaaniwa na Mungu

Habari Zinazoshabihiana
• Mwinjilisti: Wasabato wanaomsubiri Yesu wapotoshaji 22.03.2008 [Soma]
• Askofu ahofia mafisadi kupindua nchi 24.03.2008 [Soma]
• Nikichukua rushwa Mungu anichukue - Pinda 04.03.2008 [Soma]

Na Charles Mwakipesile Mbeya

MRATIBU wa Maombi wa huduma ya Tanzania Itubu Taifa, Mwinjilisti Ambokile Mwasomola, amesema kitendo cha wananchi wa Kijiji cha Kanga Chunya, kupiga mawe magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais Jakaya Kikwete, ni laana mbele ya Mungu kutokana na ukweli kuwa kiongozi huyo kuwekwa madarakani na Mungu.

Akizungumza juzi na mwandishi wa habari hii kuhusu sakata hilo, alisema wananchi hao wameonesha tabia ya ajabu ambayo kama Watanzania hususani wa Mkoa wa Mbeya hawatafanya maombi makubwa kwa ajili ya toba mbele za Mungu, ni wazi kuwa laana kubwa itashuka.

Alisema Biblia inasema mamlaka zote zinazotawala zimewekwa madarakani na Mungu na hivyo ngazi ya Rais haitakiwi kufanyiwa mchezo wa aina yeyote.

Mratibu huyo wa maombi alisema sababu kuwa walitaka kumuona Rais kamwe haitoshi kufanya fujo hizo na hivyo kinachotakiwa ni wahusika na waombaji wa Mkoa wa Mbeya, kufanya maombi maalumu kama njia ya kutubu.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika

Mwinjilisti: Mbeya kulaaniwa na Mungu

Habari Zinazoshabihiana
• Mwinjilisti: Wasabato wanaomsubiri Yesu wapotoshaji 22.03.2008 [Soma]
• Askofu ahofia mafisadi kupindua nchi 24.03.2008 [Soma]
• Nikichukua rushwa Mungu anichukue - Pinda 04.03.2008 [Soma]

Na Charles Mwakipesile Mbeya

MRATIBU wa Maombi wa huduma ya Tanzania Itubu Taifa, Mwinjilisti Ambokile Mwasomola, amesema kitendo cha wananchi wa Kijiji cha Kanga Chunya, kupiga mawe magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais Jakaya Kikwete, ni laana mbele ya Mungu kutokana na ukweli kuwa kiongozi huyo kuwekwa madarakani na Mungu.

Akizungumza juzi na mwandishi wa habari hii kuhusu sakata hilo, alisema wananchi hao wameonesha tabia ya ajabu ambayo kama Watanzania hususani wa Mkoa wa Mbeya hawatafanya maombi makubwa kwa ajili ya toba mbele za Mungu, ni wazi kuwa laana kubwa itashuka.

Alisema Biblia inasema mamlaka zote zinazotawala zimewekwa madarakani na Mungu na hivyo ngazi ya Rais haitakiwi kufanyiwa mchezo wa aina yeyote.

Mratibu huyo wa maombi alisema sababu kuwa walitaka kumuona Rais kamwe haitoshi kufanya fujo hizo na hivyo kinachotakiwa ni wahusika na waombaji wa Mkoa wa Mbeya, kufanya maombi maalumu kama njia ya kutubu.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
HUYU BADO ANAOTA KUWA JK NI CHAGUO LA MUNGU!

3. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#3
Aug 28, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0
hivi jamani kutokana na ugumu wa maisha na hali inavyokuwa mbaya kila siku polisi wanavyonyanyasa raia bila ya makosa watu wanavyokosa haki ya huduma za afya. Kuna watu walijifanya ni marafiki wa MUNGU na kumsemea MUNGU eti kikwete chaguo lake je? Kwa sasa wataweka wapi sura zao?

4. Gama

Gama JF-Expert Member

#4
Aug 28, 2011
Joined: Jan 9, 2010
Messages: 9,223
Likes Received: 1,412
Trophy Points: 280
We huwaoni kila siku na singo zao mpya?!,

5. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#5
Aug 28, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0
naona wanawaonea aibu waumini wao lakini huku ni kujipendekeza kwa viongozi wa dini kwa MIGAMBA tu hawana lolote hawa maaskofu wanaojinafkisha.

6. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#6
Aug 28, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0

Ni wanafki sana

7. Lokissa

Lokissa JF-Expert Member

#7
Aug 28, 2011
Joined: Nov 20, 2010
Messages: 7,079
Likes Received: 155
Trophy Points: 160
wengi walipongeza uteuzi wa kikwete kugombea 2005 kuanzia CCT,CET NK kama wamsema KILAINI sio yy mwenyewe alisema hiyo kauli,ika kwa sasa wameshagundua huyu jamaa alikuwa chaguo la kifisadi na sio la Mungu kwani waliomweka madarakani ni mafisadi.angekuwa chaguo la Mungu asingekaa kimya kutetea mafisadi na kutuchezea movi za kiinimacho kama JAIRO, NGELEJA,LUHANJO, rais pekee Afrika ambae anaendesha nchi bila vision ya miaka 2 mbeleni hajui anafanya nini zaidi ya kuhudhuria makongamano,kufuturisha,misiba,harusi,birthdays,kukaribisha kila mtu ikulu hata wacheza vikapu wasiokuwa na tija ktk taifa letu nk.....aialike siku moja timu ya JF IKULU pia nasi tuna mchango ktk taifa letu.lol

8. A

Amanyisye Member

#8
Aug 28, 2011
Joined: Jan 11, 2011
Messages: 23
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
walikuwa sahihi! Ni chaguo la mungu kutuonyesha yule tunaemshabikia sana kumuona yukojeili tusirudie tena.

9. V

Vonix JF-Expert Member

#9
Aug 28, 2011
Joined: Apr 23, 2011
Messages: 1,988
Likes Received: 507
Trophy Points: 280
Simba d,mada imesimama,huyo askofu Kilaini aliyekuwa mstari wa mbele kusema jk nichaguo la Mungu ameaibika bora amefichwa bukoba na serikali ya jk ndio kwanza inalituhumu kanisa hilo kuhusika na madawa ya kulevya.hilo ni pigo sana jk haaminiki.

10. Desteo

Desteo JF-Expert Member

#10
Aug 28, 2011
Joined: Jul 27, 2011
Messages: 448
Likes Received: 8
Trophy Points: 35
bado ni chaguo la Mungu kwani kwa kupitia yeye nchi hii inaingia kwenye mageuzi ambayo hatukutarajia

11. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#11
Aug 28, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0

Sana jamani

12. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#12
Aug 28, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0

Nipe gwala

13. p

peacebm Member

#13
Aug 28, 2011
Joined: Jan 31, 2010
Messages: 58
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
ataficha **** kwa mukulu

14. M

Mafie PM JF-Expert Member

#14
Aug 29, 2011
Joined: Mar 19, 2011
Messages: 1,318
Likes Received: 2
Trophy Points: 135

Pia kumbuka Mungu anaweza kukuchagulia janga kama umeshindwa kumheshimu illi uteseke na ujifunze adabu ktk maisha yako. Kumbuka Mungu aliwapatia Israel mfalme movu akawanyanyasa sana hadi wakamkumbuka Mungu ktk hayo mateso

15. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#15
Aug 29, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0

Aaagh dogo cjakuona hata siku moja humu vp mambo ha ha ha ha...

16. mkonomtupu

mkonomtupu JF-Expert Member

#16
Aug 29, 2011
Joined: Jul 5, 2011
Messages: 445
Likes Received: 22
Trophy Points: 35

yeye na wenzake waliomsupport c ndio hao wako kwenye kashfa ya madawa ya kulevya, wezi wakubwa

17. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#17
Aug 29, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,967
Trophy Points: 280
Huu ndio unafiki unatumaliza kwa kujifanya wema mbele ya viongoz wetu. Alihis atapata nafas ktk ufalme wa Kikwete.

18. KALYOVATIPI

KALYOVATIPI JF-Expert Member

#18
Aug 29, 2011
Joined: Aug 11, 2011
Messages: 1,419
Likes Received: 13
Trophy Points: 0

Alitaka nn sasa kwani uaskof wa jimbo aumtosh? Ni unafki tu hawa maaskofu wengi ni MAFIA GANG

19. Mamndenyi

Mamndenyi JF-Expert Member

#19
Aug 29, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 29,130
Likes Received: 6,615
Trophy Points: 280
no comments nina hasira

20. r

rutebukasabas Member

#20
Aug 29, 2011
Joined: Apr 18, 2011
Messages: 9
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Utawala wa kikwete umelifanya taifa hili kujua vizuri neno UFISADI. Umefungua kwa uwazi uhuru wa vyombo vya habari na kuwafanya watanzania kuona umuhimu wa CHADEMA .Bunge limefunguka na kuweza kuanika hadharani mambo mbali mbali kuanzia Richmond n.k. Huu ndo mwisho wa utwala wa CCM.
Watu hawawezi kuleta mabadiliko bila kufunguka kwa kujua matatizo yaliyopo.Kikwete ameweka wazi kuwa sera za ufisadi zimeota mizizi na utawala wake ni sehemu ya UFISADI.Hii ni hali halisi.Nguvu ya CHADEMA na vyama vingine vya upinzani inatokana na matatizo halisi yaliyopo ndani ya utawala wa Kikwete.

Loading...