Watu wa Tabora tujuzeni kuhusu ufisadi huu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu wa Tabora tujuzeni kuhusu ufisadi huu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrimi, Nov 12, 2011.

 1. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jana mkuu wa mkoa alishuhudia live jinsi jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya mpya ya Uyui lilivyochaa kwa kipindi kifupi tu tangu lianze kutumika.
  Kiukweli kuta zina nyufa na milango ipo hoi kiasi kwamba ni vigumu kumshawishi mtu mzima na akili zake kuwa limechoka hivi baada ya kutumika kwa miezi michache tu.

  Akitolea mfano, mkuu wa mkoa alisema ametembelea wananchi kijijini na kukuta milango ya nyumba zao ni bora kuliko aliyoikuta pale ofisini.

  Kwa kuwa wengine tupo mbali na mkoa huu, tunaomba weyeji wa hapo watujuze angalau wahusika wake ni akina nani.

  Nawasilisha...
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Unashangaa majengo hayo ya mkuu wa wilaya wa Uyui, you have'nt seen nothing yet; kaangalie hayo majengo ya UDOM waliyojengwa na wachina kwa pesa yetu ya NSSF ambavyo yamekwishaanza kupata nyufa hata miaka miwili haijaisha!! VIONGOZI WAPO NA WANAPITA PALE KILA LEO LAKINI WAMEZIBA MACHO NA MASIKIO KWASABABU YA 10% WANAZOHONGWA NA CONTRACTORS WA KICHINA!! Huo ndio utamaduni wa serikali ya mkweree, wanafanya watakavyo utafikiri nchi hii mali yao.
   
 3. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Bahati nzuri jengo hilo limejengwa na kusimamiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa tabora.
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Niliona jana anamuamuru engineer wa mkoa eti afuatilie wote waliohusika wawajibike, ingawa kiukweli muonekano wa usoni alikuwa amepoa sana.
  Inawezekana kweli anafahamu wahusika. Kwani intelijensia yake ina kazi gani mpaka ampe kazi ya uchunguzi engineer wa mkoa?
   
Loading...