GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,006
- 126,388
Nitoe tu ombi langu la Kipekee kabisa kwa Watu wa Itifaki ( Protocol ) hasa wale mliopo Ikulu hebu jitahidini basi muweze kumpa mafunzo ( training ) maalum ya Public Speaking Mama yetu mpenda First Lady Janet Magufuli.
Leo si mara yangu ya Kwanza kuona kila anapopewa nafasi ya kusema chochote au kuzungumza na halaiki huwa anakuwa hana la kusema sana lakini pia huwa anakuwa na aibu na hata akimaliza kuzungumza anaonekana ni Mtu anayetetemeka hivi.
Kinachoniuma kama siyo kunisikitisha huu ni mwaka wa pili sasa nyie Watu wa Protocal hapo Ikulu mpo nae huyu Mama yetu mpendwa lakini sijui ni kwanini mmeshindwa kumsaidia Mama yetu kwa hili la Yeye kutokuwa mzuri katika Public Speaking.
Najua kuzungumza katika halaiki kubwa si jambo rahisi ila kama akipewa mafunzo maalum na Yeye pia akiwa tayari basi ataweza kumudu na kuwa mzungumzaji mzuri sana. Ni jambo la aibu na si zuri pia kwa Mke wa Rais kila anapopatiwa nafasi ya kuzungumza anabaki tu kuchekacheka na kuzungumza kwa Sekunde 13 hadi 17 kisha anarudi Kitini.
Katika maisha yangu yote sijawahi kuona Mwalimu anakuwa hawezi kufanya Public Speaking ila labda Mama yetu anashindwa kwakuwa muda mwingi alikuwa anazungumza tu na Wanafunzi Watoto wa pale Shule ya Msingi ya Mbuyuni alipokuwa akifundisha kwa miaka mingi achila mbali kuwa pia alisoma hapo hapo alipokuwa Mwanafunzi miaka hiyo.
Binafsi huwa nina hamu sana pale nikiona anapewa muda wa kuzungumza na halaiki basi aje mbele na azungumze mambo mengi ya maana ili kufukia ' mashimo ' ambayo pengine Mumewe aliyasahau kitu ambacho kitazidi kufanya Watu wamuamini, wampende na waamini kuwa kweli Mheshimiwa Rais ana ' Jembe ' la uhakika.
Tafadhali Mke wa Rais Mama Janet Magufuli apatiwe haraka sana mafunzo ya Public Speaking na Yeye mwenyewe pia ajitahidi kuondokana na hiyo aibu aliyonayo ambayo kiukweli na nafasi yake ya sasa aliyonayo hapashwi kuwa nayo.
Yangu ni hayo tu na ni matumaini yangu ushauri wangu huu utazingatiwa na kuanzia siku za baadae nitamuona Mama Janet Magufuli mpya anayechangamka, anatoa madini tupu mdomoni mwake na mpambanaji kama ambavyo tunawaona Wake wa Marais wengine sehemu mbalimbali duniani.
Akhsanteni na nawasilisha.