Watu wa madili wameishia wapi?

Watu wa madili wameishia wapi?

majebsmafuru

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Posts
463
Reaction score
649
Magu kweli katunyoosha, hakuna cha dili wala madili, misheni tauni imekuwa fedheha, yale ya kusema utafute nauli tu ya kwenda tauni kurudi utakuwa umejaa mapene na hela ya kutosha msosi, nyama choma na hata kulinda meza kesho hakuna!

Ila tukubali yale yalikuwa maisha feki mno, hayarudi tupende tusipende, watu tulikuwa tunajifanyia tutakayo, kuanzia kumpiga vibao polisi, kumiliki bila woga nyara za serikali, mapene yalijaa majumbani mwetu na buti za magari kama wauza unga, tuliuza unga mpaka tukajulikana na kina El Chapo!

Unga ulihusisha kila raia, kuanzia raia wa kawaida mpaka watoto wa vigogo, tulijiunganishia mabomba ya mafuta bila woga, tuliiba na kujenga mahekalu kama vile tutazikwa humo, tuliendesha magari ya kifahari na yanayokula mafuta kama Wana Saudia!

Watu wa madili wameishia wapi?!

Tulipangisha vimada vyetu Sinza, Kinondoni na Magomeni bila kufikiria mara 2, tulipandisha bei za vyakula kwenye migahawa, nguo Boutique na kugawa hela kwa wanamuziki na wanaotuomba au kutusifia kama vile tuko Brunei!

Hahaha, kweli tukula maisha, Trafiki polisi akikohoa tu 50, mtu akitubishia lazima apigwe mkwara wa "Unajuwa mimi ni nani?" Tulitishia, tulitoa watu lupango, Mapolisi, Wanausalama, Viongozi sehemu zote muhimu walikuwa mikononi mwetu!
Kweli ambaye hakula maisha kipindi cha 2015 kurudi nyuma asage meno!

Tulivunja mifupa ile mbaya, kila aina ya Ufisadi ulifanyika, kila aina ya wizi ulifanyika, ukatili, mauaji, dhulumati, kujenga hovyo hovyo popote pale tujisikiapo!

Ndio hata Msasani kwa Mwl. Tulijenga! Ofcourse kabla ya wahusika hawajarudisha fahamu zao.

Kila aina ya maraha yaliliwa, uliza kitu gani hatukufanya utasikia hakuna...
Watu wa Madili Wameishia Wapi?!
🙁😡😕😎😵
 
Wameishia kwenye MAADILI. [emoji3]
 
Bado maisha yapo ila sasa watu wanakula kwa heshima.
 
Chamoto kinatupata, ila hatufi, tunapambana mpaka mwisho..
 
Back
Top Bottom