Watu tuna matumizi tofauti ya Facebook, leo ngoja nizungumze kwa uchache.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
21517_1084375351604876_1220385982142667868_n.jpg


Tuna matumizi tofauti ya Facebook, leo ngoja nizungumze kwa uchache.

• Kuna wale watu waliosikia Facebook kuna mademu wakali, ukiwa huko, utawapata wengi, nao wakajiunga, hawakuja kwa ajili ya kutengeneza urafiki, walikuja kwa kuwa walisikia kuna mademu wakali, nao wakawataka hao mademu.

• Kuna wale waliojiunga Facebook kwa kuwa walisikia kwamba kuna wanaume wazuri, mahandsome ambao wanaendesha magari, wana hela, wanapiga picha Kilimanjaro Hotel, kweli wakaingia Facebook na kukutana nao.

• Wengine waliingia Facebook kwa kuwa walihitaji marafiki wa kweli, kuchati nao, kupata marafiki mbalimbali, kweli wakafanikiwa.

NDUGU ZANGU,

• Facebook ni mtandao wenye urahisi kutumia kuliko mtandao wowote wa kijamii, ukiutumia vizuri, utakupa fedha, utapata fedha hata ukiwa kitandani kwako, si kwa njia mbaya, ni zile za halali kabisa, inategemea umejipanga vipi.

• Facebook ilinipa kazi, sikuwahi kufikiria ila watu walikubali nilichokifanya na mwisho wa siku nikatusua. Sikuwahi kuandika posti za matusi, kuwatangaza wasichana na utupu wao, sikuwahi kuwatapeli watu, nilichokifanya ni kile nilichokiona kwangu kuwa sahihi ambacho kitamfanya hata bosi wa CRDB awe rafiki yangu, Mkurugenzi wa Vodacom awe mshikaji wangu lakini pia hata yule dada wa kazi anayefanya kazi huko Lindi awe rafiki yangu.

• Sikuwahi kusema nimeingia Facebook kufuata mademu, sikushawishiwa na mtu kwamba nikiingia humu nitakuta mademu wakali, niliingia humu kwa kuwa nilihitaji marafiki wa kweli, wale watakaoweza kunishauri na hata wale ambao wana akili kubwa kuliko mimi ili nijijenge kwenye ubongo wangu lakini pia nijue vitu vingi.

• Nilipoingia Facebook nilijiwekea malengo yangu, nilisema acha niipende Facebook kama chakula, ila sitoiacha mpaka pale nitakapoona Facebook imenipa kitu fulani, yaani hata ikitokea siku mtu akiniuliza unapenda sana Facebook, imekupa nini, niwe na cha kumwambia.

• Amini rafiki yangu, kuna watu wengi humu Facebook wamepata kazi, kawa rafiki wa bosi fulani, wakachati-chati mwisho wa siku kapewa kazi. Unapokaa Facebook na kuandika matusi, kuwatukana watu, kuchochea ngono, kuna watu wanakuangalia, hata kama wana nafasi za wewe kupewa kazi, hawawezi kukupa.

• Kuna watu wengi wamekosa kazi, kisa tu mabosi walipopitia profile lake Facebook wamekutana na posti za ajabu-ajabu, wamekuta picha za huyo mtu kavaa nusu utupu, picha chafu ambazo ukiingia Facebook kwa simu yako wakati upo kwenye daladala na mtu akaona, ni rahisi kudhani unaangalia picha za ngono kumbe Sikujua ametoka kuposti picha yake, eti kabusti matiti, naye aonekane mrembo, eti kapiga picha kavaa sketi laini ili nguo yake ya ndani ionekane.

• Kuna watu humu wnanafanya michakato ya pesa, na kweli wanazipata na wala aihitaji elimu kubwa, ni elimu ndogo lakini utapata kile unachostahili kupata.

• Mara nyingine nimekuwa nikiwashangaa watu wanaoweka picha chafu, si kwamba hawaruhusiwi, wanaruhusiwa ila ninajiuliza kuna nini kinaendelea? Huu ni mtandao, kuna biashara nyingi, wengine ndipo pa kukamatia wateja wao na ndiyo maana wanakesha kama popo, ila kwa wale wasiojua chochote, wale wakina Sikujua, wanapomuona Baby Diva kaweka picha kabust kifua chake, na yeye kesho kafanya hivyo...Sikujua, unaiga pozi la Baby Diva, mavazi ya Baby Diva, je unajua ni kwa nini huyo yupo Facebook?

• Wengine wamepoteza muelekeo, mtu ana familia yake, kagombana na mkewe, matatizo hayo anakuja kuyaanika hadharani, wengine wameachwa, wanakuja na kusema kamwe usimwamini mwanamke/mwanaume, kisa tu yeye kaachwa. Ndugu yangu, ukitaka kuifahidi Facebook, jifanye kama ni sehemu moja ya kuenjoy, sehemu itakayokufanya ucheke hata pale unapotakiwa kulia.

• Unaweza kupata kazi kwa ajili ya Facebook lakini pia unaweza kukosa kazi kwa ajili ya Facebook. Ukitaka kuiweza Facebook, isikuendeshe, wewe ndiye uiendeshe, ikikwambia twende kushoto, iambie hapana, huko kuna matuta twende kulia.

MIMI KAMA RAFIKI YENU, KAMA MSHAURI WENU, TUWE NA MATUMIZI MAZURI NA HUU MTANDAO, NI MWEPESI KUTUMIA, ILA NI MWEPESI KUKUKOSESHA MARAFIKI NA AJIRA.
KAMA UNA SWALI...ULIZA TU.

Unaweza kushare na kuwatag mabesti zako...

Credit: Nyemo Chilongani
 
Back
Top Bottom