Watu sahihi ni wepi?

Watu sahihi ni wepi?

pipi34

Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
5
Reaction score
6
WATU SAHIHI NI WAPI?
Ni wale ambao mnabadilishana changamoto na fursa, ambao watasababisha upige hatua.
Sio mnaokutana kwenye mambo ya kupotezeana Muda na Rasilimali nyingine, wanaofurahia anguko lako, wasio na mchango kwenye unachokifanya nk.

UTAWAJUAJE?
1.Hakikisha unamjua Kiboko yako, yaan kuna wale watu ukiwaangalia na wewe unatamani kuwa kama wao ,fwatilia kila wanachofanya hata kwenye mitandao kama huwez kuwa nao Karibu, Lakin pia sio dhambi kujipendekeza kwa mtu unaona ataongeza thamani
2.Usikubali kukaa mahali ambapo hupati changamoto au washindani , yaani wewe ndo unaonekana bora, tajiri, unaakili , mzuri, nk. hapo panakudumaza Hakikisha ulipo kuna kiboko yako, ili ujifunze , lakini pia hakikisha kuna wanyonge wako ili uweze kujipima.

3.Cha mwisho
Jua ndoto yako
Panga vile vitu utafanya ili utimize.
Kisha Anza kutafuta watu sahihi wa kuisababisha iwe kweli ..
ANZA NA SOCIAL MEDIA
Pitia grup 1 baada ya lingine oanisha na malengo yako. angalia kunamchango wowote kwenye unachokifanya?
Sijasema left lakin hata ukikuta ni grup la purple amua, Kadiri unapokaa na watu sahihi utapata motisha ya Kuendelea mbele, sio watu ambao wameridika, wanaongelea anasa Muda wote, wanaokukatisha tamaa, hawakuamin, wanaumia ukifanikiwa, mnaogopana, haupo huru, Hawana faida yeyote Kwako nakwambia hawatakuacha salama Jiongeze
Punguza ushirika nao wabaki kuwa Jamaa.
Ukimaliza njoo kwenye watu binafsi, tumia hata phonebook, anza na unaowaita marafiki je, wataongeza thamani? Sijasema uwadelete lakin badili namna Ya kujihusisha nao hawataachia upige hatua, ongeza watu sahihi, boresha Mahusiano nao, hao wasio na mchango wataondoka tuu.
Lakini usiwachukie masnich ,wanaokuchukia wanaokuonea wivu hawa wape nafasi ya kutoa gesi ya chuki ilowavimbia,ndo motisha yenyewe ya kileleni.
Watakusaidia usilale.

Nina maneno matam yakukufariji Lakin hayatakusaidia kama sintakuambia ukweli, japo unauma Waliokuweka ulipo ni watu ulionao amka usiangalie watakuonaje, Usimpliz mtu kwa gharama ya Maisha yako.
Bora mkaachana hapa mkakutania kileleni

Usiachane na mtu kwa ubaya huwezi kujua kesho,mwanamke mwenye hekima hueka akiba ya maneno!! Naomba kujua kwako mtu sahihi ni yupi?
 
Mtu mwenye kuujali muda na mwenye marengo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom