Watu milioni 53 EAC maskini sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu milioni 53 EAC maskini sana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ofisa Mradi wa taasisi ya Kimataifa ya Society for International Development (SID) Aidan Eyakuze


  Watu milioni 53 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaishi chini ya mstari wa umaskini, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika ili kuinua maisha yao.

  Akiwasilisha matokeo ya ripoti ya 'Hali ya Afrika Mashariki 2012' iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mradi wa taasisi ya Kimataifa ya Society for International Development (SID) Aidan Eyakuze, alisema asilimia 38 ya wananchi wa EAC ni maskini sana na kwamba nchini Tanzania idadi hiyo imeongeza kwa milioni 4.9 hadi kufikia milioni 14.9 kutoka milioni 10 katika kipindi cha 17.

  Eyakuze alisema pamoja na ongezeko hilo kwa Tanzania, Kenya inaonekana kuwa na maskini wengi zaidi kwa kuwa na maskini milioni 18.9, Uganda (milioni 8.3) Burundi (milioni 6.3) na Rwanda (milioni 4.7).

  "Chakula cha uhakika bado ni tatizo kubwa lakini jambo la kushangaza ni kwamba tuna ardhi nzuri na tunatumia mbolea kwenye kilimo chetu, swali linabakia ni kwa nini tuna njaa, kwa nini hatuwezi kulisha watu wetu?" alihoji.  CHANZO: NIPASHE

  [​IMG]


   
 2. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Kipindi cha 17 ndio nini?
   
Loading...