Watu Milioni 13 Wanahitaji Msaada Wa Haraka DRC

Watu Milioni 13 Wanahitaji Msaada Wa Haraka DRC

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Mashirika ya kibinadamu ya umoja wa mataifa yanahitaji msaada wa dola bilioni 1,68 kwa ajili ya misaada ya kiutu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako watu zaidi ya milioni 13 wanahitaji msaada wa chakula. Kwenye ripoti yake ya pamoja mjini Kinshasa mashirika hayo yakiwemo WFP, FAO na UNICEF yamesema machafuko kwenye majimbo ya Kassai na Kivu yamesababisha ukosefu wa chakula kwenye maeneo hao na kuelezea uwezekano wa kuweko na baa la njaa ikiwa hakutokuweko na msaada wa haraka.

Mwito huo wa pamoja wa mashirika ya UNICEF, WFP na FAO umefuatia hali ngumu ya kiutu kwenye majimbo ya Kassai mnamo mwaka uliopita. Mashirika hayo yameeleza kuwa watu milioni 13 wanahitaji msaada wa haraka.

Claude Jibidar ambaye ni mwakilishi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, amesema machafuko kwenye majimbo ya Kassai yalisababisha wakaazi wa majimbo hayo kutolima kwa misimu mitatu mfululizo.

Machafuko katika majimbo ya Kassai yamechangia tatizo la njaa
Machafuko katika majimbo ya Kassai yamechangia tatizo la njaa
Kassai: Tishio la kutokea baa la njaa

Claude ameongeza kuwa: "Mwaka uliopita ulikuwa mwaka mgumu sana kwa mamilioni ya raia wa majimbo ya Kassai, kutokana na mfululizo wa machafuko, magonjwa na malisho mabaya. Hali hiyo imesababisha kuweko na tishio la baa la njaa kwenye eneo hilo. Lakini kuna pia wananchi wa maeneo mengine ambao hawana chakula kutokana na machafuko huko mashariki".

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuratibu misaada ya kiutu OCHA, limeelezea kwamba mahitaji yameongezeka kufuatia ongezeko la wakimbizi wa ndani nchini DRC. Shirika hilo limeeleza kwamba Kongo ina wakimbizi wa ndani milioni 4.3. Takriban nusu ya wakimbizi hao ni kutoka majimbo ya Kassai na waliyahama makaazi yao mwaka jana.

Mashirika hayo yanaelezea pia kwamba kwenye sekta ya kiafya Kongo ilishuhudia mwaka wa 2017 ugonjwa wa kipindupindu ambao watu 1000 walifariki na watu 55, 000 waliambukizwa.

Wanaohitaji msaada wameongezeka ndani ya miaka miwili

Nusu ya wakimbizi wa ndani wa DRC wanatoka Kassai
Nusu ya wakimbizi wa ndani wa DRC wanatoka Kassai
Kuna ongezeko la asimilia 30 ya watu wanaohitaji msaada wa chakula ukilinganisha na miaka miwili iliyopita, inaelezea taarifa hiyo ya pamoja ya mashirika ya WFP, FAO na UNICEF. Asilimia 90 ya wakaazi wa majimbo ya Kassai wanaishi kwa kutegemea kilimo, lakini machafuko baina ya jeshi na wapiganaji wa kikabila wa kamwina Nsapu,yaliyodumu miezi 10 yalisababisha watu wengi kuyahama makazi yao.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa "bila msaada wa haraka wa mashirika ya kiutu, hali ya maisha ya maelfu ya wakaazi yatahatarishwa na matumaini ya kuboresha hali hiyo yanaendelea kutoweka. Tunatakiwa kuhakikisha kwamba misaada imewafikia”.

Mashirika hayo yamehitaji dola bilioni 1,6 mnamo kipindi cha mwaka.
Chanzo: DW
 
Yatokanayo na hizi saga za DRC and the likes ni projects tu.
Toka Patrice lumumba mpaka leo pesa zinamwagwa "untold truth"
Wanaingiza 1.6USD(B) wanatoa mara mbili mpaka tatu.
 
Mwenyezi mungu awafanyie wepesi waja wake.
 
Kabila Jnr days are numbered, he is running out of options and people are tired.
Roman Catholic church is backing the country wide demonstration.
DRC is heading towards dangerously unknown route....
 
Mwenyezi mungu awafanyie wepesi waja wake.
Sidhani kama ataweza, maana wanaouhusika na yote ni binadamu kama sisi..
Ebu fikiria, madini yanayotengeneza hizi simu zetu, Ipad, Laptop, Desktop yanatoka pale, achana na almasi na dhahabu walizonazo, kuna shaba pia, nyingi mno.....
Umaskini kwanini upo pale??!! ukipata jibu basi ujuwe ni sisi wenyewe wenye rangi tofauti ndio tushutumiwe...
Mahesabu yanakataa kabisa kwa DRC kuwa maskini..
 
Sidhani kama ataweza, maana wanaouhusika na yote ni binadamu kama sisi..
Ebu fikiria, madini yanayotengeneza hizi simu zetu, Ipad, Laptop, Desktop yanatoka pale, achana na almasi na dhahabu walizonazo, kuna shaba pia, nyingi mno.....
Umaskini kwanini upo pale??!! ukipata jibu basi ujuwe ni sisi wenyewe wenye rangi tofauti ndio tushutumiwe...
Mahesabu yanakataa kabisa kwa DRC kuwa maskini..
Unayosema nikweli mkuu sema bado wanaitaji maombi sababu wako katika wakati mgumu sana.
 
Unayosema nikweli mkuu sema bado wanaitaji maombi sababu wako katika wakati mgumu sana.
Maombi hayasaidii kwa Kabila na genge lake ku share huo utajiri, maombi ni maneno na imani tu, wanachohitaji ni vitendo....
 
Back
Top Bottom