Watu hawataki kuambiwa ukweli

Magari Aina Zote

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
3,076
523
Habari za jioni wakuu, Poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa.
Leo nimekuja na swali ambalo mara nyingi huwa linanitatiza sana nikaona ni vema tukalijadili kwa pamoja hapa jamvini.
Baada ya kutafakari sana na kuishi na watu mbalimbali nimegundua kuwa watu wengi hawapo tayari kuambiwa ukweli na pia hawapo tayari kuupokea ukweli.

Tuchukulie labda mtu ni mfupi, ukimwambia yeye ni mfupi hakubali kuwa yeye ni mfupi, au labda mtu ni amelewa ukimwambia yeye ni mlevi hakubali. Labda kama hawa dada zetu unaweza kukuta siku hiyo katoka na mtoko Fulani hajapendeza, ukimwambia hajapendeza ana-mind hata anaweza akakuchukia au akanuna mwezi mzima.
Tuchukulie wenzetu wachaga ukiwaambia wanapenda pesa hawakubali.

Hivi kwa nini iko hivi??
Nimeona nililete hili kwenu tulijadili swala hili kwa pamoja maana limekuwa jipu sasa.
 
Back
Top Bottom