Watu hawakufuati wewe, bali wanafuata ulichokibeba

Watu hawakufuati wewe, bali wanafuata ulichokibeba

Joined
Jan 4, 2021
Posts
5
Reaction score
7
WATU HAWAKUFUATI WEWE WANAFUATA ULICHOKIBEBA

Wakati naanza huduma ya mitandao niliandika Ujumbe mmoja tu nilipouweka kwenye mtandao nilishangaa sana ujumbe kupata likes kama elfu moja na comments kama mia nne hivi

[emoji117]Kilichonishangaza sana ni kuona likes na comments nyingi ambazo sikuwahi kuzipata hapo kabla

Ilinisumbua sana nikawa najiuliza ni kwanini nilipokuwa napost picha zangu binafsi kwenye mitandao nilikuwa sipati comments nyingi namna hiyo? Kwanini nimepost Ujumbe wa neno la Mungu nikapata comments nyingi namna hiyo?

LAKINI KATIKA KUJIULIZA NIKAKUMBUKA MAANDIKO YAFUATAYO

[emoji828]Marko 3:7-8

7 Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Uyahudi,

8 na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu,[emoji117] waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.


Ukisoma hii habari inamhusu Yesu na Mkutano wa watu waliomufuata alipokuwa baharini

Sasa angalia hao watu walichokifuata kwa Yesu biblia inasema hivi "[emoji117]WALIPOSIKIA HABARI ZA MAMBO YOTE ALIYOKUWA AKIYATENDA WAKAMWENDEA

Kwahiyo umati huu wa watu haukumfuata Yesu kama Yesu bali ulimfuata Yesu aliyebeba kitu cha kuwasaidia

Huenda bado haujanielewa ni hivi

[emoji117]Huu umati wa watu ulimfuata Yesu baada ya kusikia habari zake za kuponya wagonjwa, kufufua wafu nk kutoka maeneo ambayo amekwisha pita kwahiyo mkutano huu ulimfuata Yesu mponyaji, mfariji, mtenda miujiza na si Yesu mwanadamu wa kawaida

Kama bado haujanielewa fuatana nami katika maandiko yafuatayo[emoji116]

[emoji828]Yohana 6:1-2

1 Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia.

[emoji117]2 Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.


Kwahiyo watu hawakumufuata Yesu walifuata miujiza, walizifuata ishara

[emoji654]Baada ya kusoma maandiko haya hata Mimi sikushangaa kuona comments nyingi namna ile nikwasababu watu walimfuata Yesu hawakunifuata Mimi!

[emoji871]Ni hivi watu hawana haja ya kukujua wewe ni nani wana haja ya kujua umebeba nini!

[emoji871]Watu hawana haja ya kufuata jengo lako la kanisa wana haja na Yesu atendaye kazi ndani ya hilo jengo, Wapo tayari kukufuata hata ukiwa unaendesha ibada zako chini ya mti wa muembe ilimradi wamuone Yesu anayeokoa hali zote za udhaifu

[emoji117]Kwahiyo kama ni mchungaji usilazimishe watu waje kanisani kwako tumia kipawa chako kwa uamifu alichokiweka Yesu moyoni mwako watu watakuja wenyewe!

[emoji871]Watu hawana haja na sauti yako wana haja na kitu unachoimba kama una sauti nzuri lakini hakuna uponyaji kwenye hiyo sauti hakuna mtu atausikiliza wimbo wako!

[emoji871]Watu hawana haja na biashara yako wana haja na ubora wa biashara yako

[emoji654]Kuna watu mnalazimisha mpendwe, mnalazimisha mkubalike na mpokelewe na watu lakini hamujiulizi mna kitu gani special cha kuwanya mpendwe au mpokelewe na watu katika jamii?

Jiulize kama Yesu asingekuwa mponyaji, Mfariji, mfalme wa Amani, Mwokozi au mtenda miujiza ni nani angemfuata?

KAMA UNATAKA WATU WAKUFUATE TUMIA NAFASI YAKO ULIYOPEWA NA MUNGU VIZURI

[emoji654]Kama ni mwalimu elimisha vizuri ueleweke watu wanufaike na mafundisho yako watu watakufuata wenyewe!

[emoji654]Kama ni muimbaji andika vitu vyenye mguso juu ya maisha ya watu kiroho uone kama hautapata mialiko ya kuimba!

[emoji654]Kama ni Dada vaa vizuri, ishi maisha ya ucha Mungu uone kama hautapata Mme mwema atokaye kwa Bwana.

Mme mwema hahitaji urembo wako, vimini vyako na makeup zako anahitaji mke mwema atokaye kwa Bwana binti usije ukasahau hili

KWA BAHATI MBAYA SANA WADADA WA SIKU HIZI WANAHANGAIKIA UREMBO WAKIFIRI WATAPATA MME KWASABABU YA UREMBO TU NDIYO MAANA HAWAOLEWI[emoji4]

[emoji871]Kama ni mfanya biashara hakikisha biashara yako ina ubora unaohitajika sokoni hautatumia nguvu kuwashawishi wateja

Kumbuka: NA MKUTANO WAKAMFUATA YESU KWASABABU WALIZIONA ISHARA!

Nikuachie swali

[emoji117]Unataka tukufuate ni sahihi kabisa tutakufuata lakini je una nini? tukikufuata tutapata nini kwako?

Mungu awabariki sana[emoji120]

WhatsApp 0657117595

Mwl. Joseph Leonard
 
If your are thinking straight, ^wewe^ & ^ulichobeba^ are almost inseparable components. To put it more succinctly, wapo watu ambao wamebeba ulichobeba lakini kamwe asilani hawafuatwi ama hawawezi kufuatwa na watu wale wanaokufuata au ambao wangekufuata wewe. Nikirejea nitaongeza volume.
 
Sawa Mkuu na Mimi nakupa like ingawa sijui Kama utapata Kama ulizopata insta.

Tatizo hapa siyo insta, wanaofeki maisha hapa JF ni wachache Tena watoto.

Kwa hiyo hawatoi like kinafiki, ukipata like moja hapa Ni sawa na kumi za Insta.
 
Back
Top Bottom