Watu hawa ni hatari kuiba pesa kwenye Tigopesa

Nndu wa Selote

JF-Expert Member
Jun 21, 2012
733
520
Wadau naomba niwashirikishe jambo hili ambalo limenishangaza hasa baada ya kuwapigia kampuni ya TIGO wakapiga danadana bila kutoa majibu yanayoridhisha.
Kuna Mtu au watu wana namba za Tigo, wanakupigia simu wanajitambulisha kuwa wanapiga simu kutoka TIGO na kwamba wanataka kukuboreshea huduma ya Tigo WEZESHA, hivyo wanakusajili na wakishakusajili utapata bonus ya Tshs 50,000 na muda wa hewani wa mwezi mzima.
Wanakupa namba na kukupa maelekezo. Ukishaingiza ile namba pesa yote au sehemu ya pesa uliyonayo kwenye Tigo pesa inachukuliwa.
Dada mmoja ofisi jirani alipigiwa simu hiyo na baada ya kufuata maelekezo kwa kuingiza namba b50fd87d alipokea ujumbe kuwa Pesa imefanikiwa kutumwa kwa RASHID MFAUME, 0716 704327 kiasi Tshs.1,000,000. Immediately aliwapigia Tigo lakini hawakuchukua hatua za kuzuia ile pesa. Aliondoka kuelekea ofisi za Tigo lakini akiwa njiani alipata message nyingine kuwa Pesa imefanikiwa kutumwa kwa huyo huyo Kiasi Tshs. 600,000.
Wakati huo huo RASHID MFAUME, 0716 704327 akajinunulia muda wa maongezi kutoka kwenye account ya dada mwingine (jina ninalo) Tshs. 2,700 ambazo ndo kiasi pekee kilichokuwepo.
Mtu mwingine mwenye namba 0719 004 299, FRANK JOHN, akampigia dada mwingine akatoa maelezo kama yale ya MFAUME akafanikiwa kumwibia Tshs. 14,000 ambazo ndicho kiasi kilichokuwa kwenye Tigo Pesa.
NIKIANGALIA HAYA MAZINGIRA NAHISI KUNA UHUSIANO WA KARIBU NA WAFANYAKAZI WA TIGO WENYEWE !!! WOTE WALIOIBIWA WANAFANYA KAZI JENGO MOJA OFISI TOFAUTI, KAMPUNI TOFAUTI. jE HAO AMBAO HATUWAFAHAMU NI WANGAPI WAMESHALIZWA KWA MTINDO HUU ???
 
SP hawa wabongo ni wezi sana, na TCRA huwa hawatoi quick response juu ya matatizo ya namna hii. Wanaseheria hebu mtujuze haki hapa inaweza patikanaje???
 
Utapigiwaje simu uambiwe unaboreshewa na wewe uamini..............?........hawajui ofisi za tigo..........?
 
Hao watakuwa wanatoka hukohuko tigo, wanazijua vizuri sana system hizo ndio maana wanaiba.
 
Mie nilipata ujumbe huo kutpka namba 0789453335 kwenye namba yangu ya tigo.

Nilichojibu ni k...u...m...a...m..a...m...a...yo nikaachana nao.

"+12063171706:YOUR MOBILE NO HAVE WON($550,000.00)COCA-COLA FIFA WOMEN'S WORLD CUP CANADA TO CLAIM IT SEND UR DETAILS TO EMAIL:womansworldcup@outlook.com"

FIFA WOMEN sijawahi hata kuiangalia kwa bahati mbaya. Iweje nishinde pesa yote hiyo kirahisi namna hiyo kuzidi hata ile aliyopata Idris. Wangese sana hao.
 
Hivi ile sheria yao ya wizi wa mitandaoni haijatungwa hadi leo?. Au TCRA wana maslahi na huu wizi wa kwenye mitandao?. Ni kama mswada ulisomwa kwa mara ya kwanza juzi kati kwenye bunge la escrow vile!. Poleni mliofikwa na majanga kwani tigo hawatawalipa kwa kuwa hakuna sheria inayomlinda mlaji katika nchi hii ya majanga.
 
halafu yule february,waziri wa wizara husika nae anataka urais wakati hata hii kazi rahisi ya kudhibiti haya kashindwa,kutwa kucha yeye na facebook na Twitter.haki ya mama mi habari za rais kijana msiniletee kabisaaaa
 
Kwanza nashukuru sana matapeli;kwan wanaishi mjini kwa akili ndogo sana bila nguvu!zaidi wanatumia ujinga wako

Pili kulaumu tigo;ni ujinga mwingine.Unaendesha gari kwa spidi ukipata ajali unalaumu kiwanda cha magari!.
 
Napata Picha wadau naskia Kuna lina za tigo huuzwa elf 50.na wawezakuta mtu1 ana line zaidi ya 100 na Kila line huingiza elfu 14 kwa cku.najiuliza Hawa wanacheza mchezo gani km c wizi wa mitandaoni!!
 
Tuepuke Promo za kuambiwa umeshinda wakati hukushiriki shindano... kwa wale tulioanza na simu za ttcl, mobitel,...nk laini zilikuwa na bei na vocha ni kwa dola, siku hizi waziri na wenziwe sms bure, fb bure,twita bure, kujiunga mitandao yote- bei poa, wengine wanajiungia kwenye vyuo halafu wanarudi uraiani,,, wanaibiwa kirahisi- kuangamia kwa kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom