Munyaluganda
Member
- Jul 13, 2022
- 7
- 21
Wakati nikiwa darasa la saba tulikuwa na mtihani uliokuwa ukijumuisha shule zote za kata ulioitwa “KALABAZOLA”. Neno hili ni neno la Kisubi lenye maana halisi ya Kiswahili TUTAWAONA kwa sababu nilisoma kijijini sana hata lugha ya Kiswahili kwetu tuliiona kama lugha ya wageni kwa sababu hata kujitetea kwa Mwalimu mkuu tulijitetea kwa kimila.Shule saba ndani ya kata yetu zilishiriki.Katika mtihani huo nilipata alama 162 kati ya alama 250 zilizohitajika,wenzangu wote walipata alama chini ya 100. Mwalimu wangu wa Taaluma alipoleta matokeo hayo alinitazama kisha akaniambia “Umekuwa wa kwanza kati ya kundi kubwa la wajinga”.
Ukweli nilihuzunika sana kwa maneno hayo ya Mwalimu wangu wa Taaluma kwa sababu mimi nilijiandaa kupokea zawadi nyingi na maneno mengi mazuri ya pongezi ila haikuwa hivyo.Mimi kwa fikra zangu niliendelea kuamini kwamba ndo Mwamba wa Kata yetu richa ya maneno hayo na kuamini kwamba Mtaaluma wangu amekaa kimchongo tu ana undumilakuwili.
Sasa Mwamba wa Kata nilipomaliza darasa la saba mzazi wangu alinipeleka katika moja ya shule bora hapa Tanzania iitwayo Kaizilege kwa masomo yangu ya upili wa chini (o, level). Shule hii huwa haitoki 3 bora kitaifa kila mwaka. Kati ya wanafunzi 80 tuliokuwa kidato cha kwanza mimi nilishika nafasi ya 78 katika matokeo ya kumaliza muhula wa kwanza. Wanafunzi wengi wanaosoma shule za bweni hufurahia sana kurudi nyumbani wakati wa likizo ila kwangu ilikuwa kinyume chake.
Ndipo nilitambua kwamba, siku zote usijione kuwa wewe ni bora kuliko wengine zaidi geuka nyuma uangalia kundi ulilo nalo yawezekana kabisa ukawa kama mimi nilipokuwa nikiwaongoza wajinga wenzangu.