Watu binafsi wanaofanya biashara ya kukopesha kwa riba, wana riba kubwa,hawalipi kodi na hakuna sheria inayowabana

Angalau kwa Mara ya kwanza umeleta mchango positive. Maendeleo hayana chama
Kwa kweli katika mada hii, nami naungana nawe kupongeza 'Salary Slipi', lakini mbona hata 'like' tu umeshindwa kumpa? Nawe tunasubiri siku moja ulete mada ya 'kutuunganisha pamoja' kama hii aliyoleta leo 'slip'. Naona 'cocochanel', yupo hapo pembeni kwako akishangilia, lakini hana ubavu wa kumshanglia 'slip' hata mara moja tu hii!
 
Umesajili hii biashara? Una uhakika na unacho kisema? Una weza nipa kanuni za sheria ya kukopesha? Una fahamu sheria ina ambatana na kanuni zake?
Mbona ungekuwa umefanya jambo la maana sana 'Chillah' kama ungeweza kuweka kanuni na sheria yenyewe! Hii ingetusaidia wengi tusioifahamu, na mada hii ingenoga sana!

Nimesoma mengi uliyoweka hapa, kidogo natoka na hisia ya kwamba unakosa 'sensitivity' ya mengi yanayosemwa na hawa unaojibishana nao humu.

Kama sheria na kanuni zake ipo, na bado kukawa na hawa 'vishoka' wakafanya wanvyopenda nje ya sheria hiyo na wahusika wa utekelezaji wa sheria hiyo bado wakawa hawatimizi wajibu wao - hivi ni haki kweli kuwalaumu wahanga wanaoumizwa kwa kushindwa kutekelezwa kwa sheria ile? Nina hakika kuna watu kila mwisho wa mwezi wanapokea mishahara, tena minono sana, ambao kazi yao ni kuhakikisha hizi sheria zinafuatwa. Kwa nini tusiwalaumu hawa kwa kushindwa kutimiza wajibu wao?

Huyu 'mhanga' anayelazimishwa na 'hali halisi' inayomkabili na kwenda kujisalimisha kwa mikopo ya aina hii, tukose kabisa 'sensitivity' ya kujua kinachomsukuma hadi kujisalimisha huko? Sisi kweli hatujawahi kabisa kukutana na 'hali' iliyotulazimisha kufanya jambo ambalo kwa hali ya kawaida kabisa tusingelifanya? Tena basi, siyo kwamba amevunja sheria kwenda kuchukua huo mkopo wenye riba kubwa, kama ni kweli sheria na kanuni zipo kama unavyoelezea hapa zinazosimamia aina hii ya mikopo.

Tuwekee sheria na kanuni zake, kama unazo.
 
Nchi hii kuna watu wanatengeneza faida kubwa kwa biashara ya kukopesha lakini watu hawa hawalipi kodi na hii ni kwasababu hakuna sheria inayodhibiti biashara hii ya kukopesha ingawa baadhi wanakopesha kwa mikataba maalumu tena inayoshuhudiwa na mawakili.

Hivi sasa kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu,watu kutafuta mitaji ya kuendeleza biashara zao,n.k,watu hulazimika kutafuta mikopo mitaani ambako riba ni asilimia kati ya 20,25,30 mpaka asilimia 40.

Kwa mfan,.mtu akikopa shilingi laki moja ndani ya siku 30,basi mkopaji hutakiwa kurejesha kiasi cha shilingi kati ya 120,000 mpaka 140,000 kwa mwezi kutegemeana na riba ya mkopo.

Baadhi ya watu hawa wanakuwa na biashara zinazotambulika kama maduka,grocery,n.k ila hapo hapo wanakuwa na biashara hii isiyo rasimi ya kukopesha ambako wanatengeneza hela nzuri tu kupitia shida na matatzo ya watu katika jamii inayowazunguka.

Mtu ana leseni ya kuuza duka, na hapo hapo anafanya na biashara ya kukopesha, jambo ambalo sidhani kama ni sahihi.

Ukiacha watu binafsi, zipo pia taasisi za kifedha zinazotambulika na ambazo zinazotoa mikopo ila nazo huwa na mikataba inayoficha kiasi halisi cha riba wanazotoza na wengine huwa hawatoi mikataba kwa wateja wao na bila shaka hufanyi hivi ili kujiweka salama kwani wanajuawa wanachokifanya sio sahihi.

Ili kudhibiti biashara hii na kuhakikisha na hawa watu nao wanalipa kodi,serikali ije na sheria ya kutaka kila anaefanya hii biashara anasajiliwa,analipa kodi na mikataba anayoitoa kwa watu iwe inakaguliwa na mamlaka husika na zaidi iwe ni kosa kwa mtu kufanya biashara hii pasipo kusajiliwa.

Pia,sheria iweke ukomo wa hizi riba kwani zinaumiza watu na zaidi zinaleta umasikini kwa watu na kuwa kikwazo katika vita ya kupambana na umasikini.

Najua ni biashara ambayo inaweza kuwa ngumu kuidhibiti ila tukiwa na sheria, watu wataogopa na hata mtu akishindwa kurejesha, mkopeshaji ni lazima atatumia busara kudai hela yake kwani wakishindwana na kupelekana katika vyombo vya sheria, mkopeshaji nae atakuwa ni mtuhumiwa moja kwa moja kwa kukiuka sheria na hivyo wataogopa.

Kama tutakuwa na mtazamo kuwa, biashara hii inafanyika kwa siri au kwa makubaliano kati ya watu wawili au zaidi na hivyo itakuwa ni vigumu kuidhibiti,basi tujiulize kama mtazamo ungekuwa ndio huu katika biashara kama zile za madawa ya kulevya ambayo nazo hufanyika kwa siri?

Tatizo mojawapo kubwa la nchi hii ni kuwa, kuna watu wanafanya biashara au shughuli zinazowaingizia faida kubwa tu ila hawalipi kodi na badala yake ni watu wachache ndio wanaolipa kodi katika nchi hii.

Mifano ya watu wengine wanaofanya kazi au biashara inayowaingizia fedha nyingi ni madalali wa viwanja,nyumba,mashamba,n.k na hii ni kwasababu hakuna sheria inayosimamia biashara wanayoifanya na kama ipo basi haisimamiwi ipasavyo.

Matokeo ya watu wengi kufanya kazi au biashara pasipo kulipa kodi, ni mzigo huo wa kulipa kodi ya serikali kubebwa na wafanyabiashara waliosajiliwa na watumishi wa umma wanaokatwa kodi kubwa kila mwisho wa mwezi katika mishahara yao na ndio hawa hawa tena huenda kukopa mitaani kwa riba kubwa kutoka kwa watu ambao baadhi hata kodi hawalipi kutokana na kufanya hii biashara isiyo rasimi.

Laba nimalizie kwa kuuliza hivi:

Je,katika nchi za wenzetu,hali ni hii hii ya watu wengi kufanya biashara au shughuli kama hizi pasipo kutambuliwa rasimi na kutolipa kodi serikalini?

Au pia tujiulize kama ni sahihi kulaumu TRA kwa kutoza kodi kubwa wafanyabiashara, alafu ukaona ni sahihi mtu mwingine(ukiwemo wewe mfanyabiashara unaeilamu TRA) kutoza raia mwingine riba ya asilimia 20 mpaka 40 tena pasipo hata kulipa kodi?

Hata hivyo,wakati tunahimiza watu walipe kodi,serikali ziache matumizi ya hovyo ya kodi zetu kama haya yanayotokana na sheria ya uchaguzi ambapo mtu hata akijiuzulu kwa kuunga mkono juhudi, baada ya muda serikali inalazimika kuitisha uchaguzi kwa gharama kubwa(matumizi mabovu ya kodi za wananchi masikini).

Kwanza ulazimishwi wala kuvutwa Kwa kamba ni shida ndo umfanya MTU akakope atatue shida zake.PILI hakuna MTU asiyelipa kodi kila MTU ulipa kodi kadri anavyonunua mahitaji yake ni faida Kwa muuzaji ambae apatapo faida ulipa kodi
 
Sheria ipo tena kali
Ni marufuku kufanya biashara ya kukopesha bila ya leseni ya BoT,sheria ya fedha 2019,kasome sambamba na 2007
Huo ni utakatishaji pesa
Sheria bila usimamizi haina maana yoyote.

Hili jambo hakuna analifuatilia na ni kwasababu watu wamekaa kimya na wanaotakiwa kusimamia utekelezaji wa sheria nao wako kimya.
 
Hata hivyo,wakati tunahimiza watu walipe kodi,serikali ziache matumizi ya hovyo ya kodi zetu kama haya yanayotokana na sheria ya uchaguzi ambapo mtu hata akijiuzulu kwa kuunga mkono juhudi, baada ya muda serikali inalazimika kuitisha uchaguzi kwa gharama kubwa(matumizi mabovu ya kodi za wananchi masikini).

Nimependa hii conclution..
 
Upo sahihi kabisa, tena unaambiwa dhamana upeleke vitu vya kama TV, kompyuta, gari. ukikopa milioni urudishe milioni na laki mbili ndani ya mwezi. Ni shida sana..
Kwakweli huu ni wizi kabisa na ni unyonyaji wa wazi ila serikali iko kimya tu!!
 
Sheria bila usimamizi haina maana yoyote.

Hili jambo hakuna analifuatilia na ni kwasababu watu wamekaa kimya na wanaotakiwa kusimamia utekelezaji wa sheria nao wako kimya.
Mkuu ulienda kuripoti ukapuuzwa?
Siku zote utendaji wa pole popote duniani unategemea kutonywa na wasamaria wema
 
Kwakweli huu ni wizi kabisa na ni unyonyaji wa wazi ila serikali iko kimya tu!!
Na shida yote hii ni kuacha mabenki yatoze watu riba kubwa na masharti kibao ya kukopesha, hivi kwa nini mabenki na taasisi zilizosajiliwa zisitoe hii mikopo midogo midogo (microfinance) angalau kwa riba na masharti nafuu au ndo kila mtu anaachwa apambane na hali yake. Umezungumzia pia swala la kodi, kuna biashara nyingi tu mfano, ya kupangisha nyumba haziko regulated kiasi kwamba serikali haikusanyi kodi hata senti na watu wananyanyaswa na hao wenye nyumba. Mtu anatoza pango la nyumba kodi anayojisikia na anataka kuanzia miezi sita hadi mwaka, hutaki unaacha. Na hatujasikia serikali ikipendekeza watu walipwe mshahara wa miezi sita au mwaka mzima, iweje iruhusu watu watozwe kodi ya pango kwa miezi 6-12. Tukiogea humu kwamba serikali haifanyi regulation kwenye maeneo mengi na kusababisha ugumu wa maisha kwa watu wengi na hata serikali kushindwa kukusanya kodi kwenye maeneo mengi na kuwabambikizia kodi kubwa wafanyakazi, kuna watu wanatokwa mapovu eti tunawaharibia. Nilileta mada humu kuhusu serikali kudhibiti bei na upatikanaji wa nafaka watu wakaanza kunishambulia eti nawaharibia. Sasa unajiuliza, ni wapi huko serikali inapotakiwa ifanye udhibiti, halafu wao waachwe wafanye wanavyotaka unakosa jibu.
 
Mbona ungekuwa umefanya jambo la maana sana 'Chillah' kama ungeweza kuweka kanuni na sheria yenyewe! Hii ingetusaidia wengi tusioifahamu, na mada hii ingenoga sana!

Nimesoma mengi uliyoweka hapa, kidogo natoka na hisia ya kwamba unakosa 'sensitivity' ya mengi yanayosemwa na hawa unaojibishana nao humu.

Kama sheria na kanuni zake ipo, na bado kukawa na hawa 'vishoka' wakafanya wanvyopenda nje ya sheria hiyo na wahusika wa utekelezaji wa sheria hiyo bado wakawa hawatimizi wajibu wao - hivi ni haki kweli kuwalaumu wahanga wanaoumizwa kwa kushindwa kutekelezwa kwa sheria ile? Nina hakika kuna watu kila mwisho wa mwezi wanapokea mishahara, tena minono sana, ambao kazi yao ni kuhakikisha hizi sheria zinafuatwa. Kwa nini tusiwalaumu hawa kwa kushindwa kutimiza wajibu wao?

Huyu 'mhanga' anayelazimishwa na 'hali halisi' inayomkabili na kwenda kujisalimisha kwa mikopo ya aina hii, tukose kabisa 'sensitivity' ya kujua kinachomsukuma hadi kujisalimisha huko? Sisi kweli hatujawahi kabisa kukutana na 'hali' iliyotulazimisha kufanya jambo ambalo kwa hali ya kawaida kabisa tusingelifanya? Tena basi, siyo kwamba amevunja sheria kwenda kuchukua huo mkopo wenye riba kubwa, kama ni kweli sheria na kanuni zipo kama unavyoelezea hapa zinazosimamia aina hii ya mikopo.

Tuwekee sheria na kanuni zake, kama unazo.
Soma tena boss... Je, ni haki mhanga kuvunja sheria kisa shida zako? Ila ukitatua shida yako una anza kujua sheria kuwa aliye kukopesha ana fanya biashara kinyume na sheria, wakati ana kukopesha hakuwa ana vunja sheria....

Bado hoja sija ielewa hapa... Wananchi ndio tunao vunja sheria tuna penda njia za panya bila kujua hatari iliyopo...

Pata muda kuelimisha hawa wavunjifu wa sheria...
 
kweli mtaani watu wanakopesha pesa ila pia risk ni kubwa, tatizo ni kwamba ili ukope bank mashart ni mengi lakini pia wengine hawana vigezo vya kukopesheka na bank lakin pia uharaka wa mkopo wenyewe, unapiga simu tu hela inakuja illa sio kila mtu anakopeshwa
 
Na shida yote hii ni kuacha mabenki yatoze watu riba kubwa na masharti kibao ya kukopesha, hivi kwa nini mabenki na taasisi zilizosajiliwa zisitoe hii mikopo midogo midogo (microfinance) angalau kwa riba na masharti nafuu au ndo kila mtu anaachwa apambane na hali yake. Umezungumzia pia swala la kodi, kuna biashara nyingi tu mfano, ya kupangisha nyumba haziko regulated kiasi kwamba serikali haikusanyi kodi hata senti na watu wananyanyaswa na hao wenye nyumba. Mtu anatoza pango la nyumba kodi anayojisikia na anataka kuanzia miezi sita hadi mwaka, hutaki unaacha. Na hatujasikia serikali ikipendekeza watu walipwe mshahara wa miezi sita au mwaka mzima, iweje iruhusu watu watozwe kodi ya pango kwa miezi 6-12. Tukiogea humu kwamba serikali haifanyi regulation kwenye maeneo mengi na kusababisha ugumu wa maisha kwa watu wengi na hata serikali kushindwa kukusanya kodi kwenye maeneo mengi na kuwabambikizia kodi kubwa wafanyakazi, kuna watu wanatokwa mapovu eti tunawaharibia. Nilileta mada humu kuhusu serikali kudhibiti bei na upatikanaji wa nafaka watu wakaanza kunishambulia eti nawaharibia. Sasa unajiuliza, ni wapi huko serikali inapotakiwa ifanye udhibiti, halafu wao waachwe wafanye wanavyotaka unakosa jibu.
Hii nchi karibu kila kitu kinakwenda hovyo hovyo kwasababu waliopewa dhamana hawana ubunifu,hawana maarifa na kazi kukaa maofisini tuna zaidi hawataki kujifunza kutoka kwa wenzetu walioendelea.

Kingine ni kuwa,watu wengi wenye maamuzi wanashika nafasi za juu serikali na ndio wanaolipwa mishahara mizuri na marupurupu kibao hivyo shida wanazopata wananchi wa kawaida wao haziwahusu na pia wamesahau walikotoka.

Waziri au katibu mkuu ambae karibu kila kitu analipiwa na serikali ikiwemo nyumba ya kuishi, leo anaweza kuelewa athari ya mtu kutakiwa kulipa kodi ya miezi 6 au mwaka?

Wacha maisha yaendelee kuwa magumu watu wakichoka kuna siku wataingia mabarabarani kutaka mabadiliko na hapo ndio wenye mamlaka watatia akili na kujua ni nani hasa boss/mwajiri wao.
 
Soma tena boss... Je, ni haki mhanga kuvunja sheria kisa shida zako?
Sheria ipi, iko wapi. Mbona tunazungushana tu hapa?

Kama sheria ipo, iliwekwa ya nini kama haisimamiwi na kufanya kazi kama ilivyotakiwa.
Mbona umekazana sana kumlaumu mkopaji na hushughuliki na mkopeshaji, ambaye ndie mharifu namba moja.
 
Inawezekana huyu jamaa nae ni mmoja wa watu anaefanya biashara hii ya kufaidika/kujinufaisha na matatizo ya watu.
 
Huyu ni 'Salary Slip'?, au jina kakodisha!

Niseme, ni mada nzuri inayostahili kupewa mjadala wa maana.

Kama 'Mmachinga' muuza karanga zenye mtaji wa Tsh 5,000/ anatakiwa kuwa na kitambulisho cha Tsh 20,000/ kwa mwaka, pasi shaka yoyote, hawa ma-'shylock' nao wanatakiwa wawekwe kwenye utaratibu wa kulipa kodi.

Umeeleza kwamba ni biashara isiyo rasmi; ikiwa na maana kwamba haitambuliki serikalini. Itakapotambulika tu, sina shaka wahusika wataandamwa ipasavyo. Wanaovuna sasa, acha wavune, hadi hapo serikali itakapozinduka.

Huko majuu, nijuavyo mimi, zipo kampuni zinazofanya biashara ya kukopesha, mbali na Benki za kawaida. Lakini hawa, kama zilivyo biashara nyinginezo, hawana nafasi ya kufanya biashara hii chini kwa chini na Kaizari asijue. Ni swala la muda tu, nasi tunaelekea huko. Mwishowe tutafika mahali ambapo mtu huwezi ukapata tu hela ya pembeni bila ya kuilipia kodi.

Hebu fikiria mfano huu: Hapa kwetu leo hii naweza kwenda dukani kwa Mangi hapa jirani yangu. Tumewekeana utaratibu kwamba, wakati nikiwa nimechacha ile mbaya, hasa kuanzia kwenye tarehe za 12 hivi na kuendelea, Mangi ataniweka daftarini kwake kwa mahitaji yangu yote, ili mama na watoto wapate kupeleka mkono kinywani na kwenda chooni. Inapogonga tu tarehe 28 na ushee, Mangi anapata haki yake, na mambo yanaendelea kama kawaida.

Kwa bahati nzuri,Mangi ni mtu mzuri katika jamii yetu, kwa sababu hatozi ziada juu ya faida anayoitegemea katika bidhaa zake. Bila shaka, Mangi angependa kuweka cha ziada katika mipango yetu hiyo, tungeweza pia kuelewana na tukaendelea na utaratibu wetu huo mpya.
Sasa sijui katika hili nalo mleta mada angesema lipi? Ninaelewa kabisa umhimu wa kupewa 'receipt' katika mauzo/manunuzi yoyote yanayofanyika kati yetu. Je, bado hapatakuwepo na mwanya wa Mangi kupata ziada ya kile kilichotazamiwa? Mimi mnunuzi, ujue pia nafaidika na mpango huu, hata kama ninalazimika kulipa ziada kidogo (service fee)?
Yapo mengi sana ambayo bado yanahitaji kufanyiwa taratibu za urasimishaji katika mipango ya maendeleo yetu. Tutafika tu, hatua kwa hatua.

Hiyo biashara (isiyo rasmi) ya kukopesha ningependa kuifanya. Lakini, je, usalama wake upo? Akikataa kulipa je? Utakwenda mahakamani kushtaki, na huku huna kibali maalum cha kufanya biashara hiyo?
Iyo ni kuwa mtu anakupa mali yake yenye value zaidi ya mkopo anaotaka kuchukua. Akishindwa kulipa hata huangaiki naye ni kama vile mmeuziana. Yeye kachukua pesa, wewe unachukua malim
 
mkuu ni hivo hivo, hiyo document inaitwa customer portfolio. Siku una renew leseni lzm uataouch, mimi naendandga kuchukua leseni pale Wizara ya viwanda na biashara kupitia BRELA mwaka wa 5 mfululizo huu. kwa hiyo naandika nachojua na ndio utaratibu wa pale, japo kulingana na mswada uliopelekwa /utakaopelekewa utaipa BoT authority ya kutoa leseni na sio BRELA tena. Hii document inazisaidia malmlaka kujua jinsi firm inavyojiendansha from the scratch, mpaka inavyokua ili kuendana na ongezeko la kodi.
Asante nazani watakuwa wameelewa...

Kiongozi fafanua hapa... La sivyo na wewe itabidi utembelee mamlaka usika ukapate taarifa kamili...

Hapa kuna uhitaji wa maelezo ya kina...
 
Back
Top Bottom