Tatizo la ajali si mwendo kasi tu, uwezo mdogo wa madereva wengi na pia forged driving licences pamoja na ufundishwaji duni! Nimewahi shuhudia makutano ya barabara ya Mwenge mwanafunzi kwenye gari la Victoria driving school akiwa na mkufunzi wake akivuka taa nyekundu bila wasiwasi ilhali madereva wengine wakiwa wamesimama, unategemea nini mtu kama huyo akipewa usukani wa basi?
Utawala wa sheria ni muhimu sana jamani, hebu fikiria jamii nayo inasema ukiendesha kwa kufuata sheria utagongwa! Jamani tunahalalisha wenyewe maasi halafu tukija kusikia watu wamekufa kwenye ajali tunabaki kusema mwendo kasi!
Barabara nyingi ni finyu ila ukiwa dereva makini bado utafika salama.
Poleni wafiwa.