Watu 44 wadakwa kwa kushambulia wanawake

Watu 44 wadakwa kwa kushambulia wanawake

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
kamanda.jpg

Siku chache baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za wanawake wanne waliojeruhiwa kwa kuchomwa moto na wakazi wa Kijiji cha Mwamabondo, Kata ya Loya wilayani Uyui wakituhumiwa kumuua mganga wa kienyeji, Mafumba Tiwilasi, polisi imewakamata watu 44wanaodaiwa kuhusika na tuhuma hizo.

Akizungumza baada ya kufika katika hospitali walikolazwa wanawake hao ambao ni Elizabeth Kashindye (47), Manungwa Lutema (45), Rahel Mikomangwa na Maria Sahani (49), Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Wilbroad Mutafungwa aliwaeleza kuwa watu 44 wanashikiliwa kwa tuhuma za kujichukulia sheria mikononi huku akieleza msako bado unaendelea kwa wengine.

Mutafungwa aliwapongeza askari wake kuwahi na kuokoa maisha ya wanawake hao huku pia akitoa pongezi kwa madaktari na wauguzi wanaowatibu.

Alisema mbali ya kuhakikisha usalama wao katika wodi wanayotibiwa, pia wataangalia namna ya kuwasaidia baada ya kupona kwa vile itakuwa sio salama kurudi kijijini kwao wakati huu.

Wakizungumza na gazeti hili wakiwa wamelezwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete, walisema waliteswa na kuumizwa kwa jambo ambalo hawalielewi.

Lutema ambaye ni mke wa marehemu Mafumba Tilawisi (70) aliyekuwa mganga wa kienyeji kijijini hapo, alituhumiwa kumuua mumewe kwa njia za kishirikina kwa kushirikiana na wanawake hao.

Alisema alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa fimbo kwenye makalio, mikononi na mgongoni na baada ya kuona anaweza kuuawa aliwataja marafiki zake watatu ambao ni Kashindye, Mikomangwa na Sahani.

Hata hivyo mke huyo wa marehemu alipata bahati ya kutochomwa moto katika baadhi ya maeneo ya mwili wake kama wenzake akiwamo Sahani aliyeunguzwa hadi sehemu zake za siri.

Kashindye alisema akiwa mtupu huku akiwa amefungwa kamba alipigwa na kuunguzwa mgongoni akitakiwa kueleza uhusika wake katika kifo cha Mafumba kwa vile alitajwa na mke wa marehemu na yeye kusema haelewi chochote. wanawake walifanyiwa ukatili huo Septemba 17 wakituhumiwa kumuua Mafumba aliyefariki ghafla Septemba 16

Chanzo: Mwananchi
 
Nazani licha ya kutokuwa na dini na elimu sahihi basi hata akili za kuzaliwa hawana kweli wacha wafu wazike wafu wenzao
 
Back
Top Bottom