John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Watu 40 walioandika Biblia
Biblia, kitabu kikamilifu na kitakatifu, kimeandikwa na waandishi zaidi ya 40, kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Ndani ya biblia kuna taarifa zinazohusu maisha ya watu zilizobeba sauti ya Mungu nyuma yake. Pia, kuna taarifa za mataifa mbalimbali, pia zenye kubeba sauti ya Mungu nyuma yake. Lakini zaidi sana kuna nabii za wakati ujao.
Zaidi ya waandishi binadamu, Biblia iliandikwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu.
Kitabu cha 2Timotheo 3:16 kinatuambia kuwa Biblia ni PUMZI ya Mungu.
Mungu aliwaongoza waandishi binadamu wa Biblia, ili, huku wakitumia mitindo ya uandishi wao wenyewe wa haiba, wao bado walinakili lile hasa ambalo ni lengo la Mungu. Biblia haikuamriwa na Mungu, lakini iliongozwa kikamilifu na Mungu, kupitia Roho Mtakatifu.
Biblia iliandikwa na takriban watu 40 wa kada mbalimbali katika kipindi cha miaka 1,600.
Licha ya kuandikwa na waandishi mbalimbali kwa muda wa miaka 1,600, Biblia haijichanganyi yenyewe na haina makosa yo yote. Waandishi wote wameonesha mitazamo yao mbalimbali, na kila mmoja ameandika kwa mtindo (style) wake, lakini wao wote wanamtangaza yule Mungu mmoja wa kweli, na hiyo njia moja ya wokovu ya Yesu (Yohana 14:6, Matendo 4:12).
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali. Katika vitabu vya Biblia, baadhi vimetaja majina ya waandishi wa vitabu hivyo.
Hapa chini pameoneshwa majina ya waandishi na vitabu walivyoandika.
VITABU VYA AGANO LA KALE
1. Amosi: kitabu cha Amosi
2. Danieli: kitabu cha Danieli
3. Daudi: kitabu cha Zaburi (zaburi 75 kati ya zaburi 150)
4. Ezekieli: kitabu cha Ezekieli
5. Ezra: kitabu cha Ezra
6. Habakuki: kitabu cha Habakuki
7. Hagai: kitabu cha Hagai
8. Hosea: kitabu cha Hosea
9: Isaya: kitabu cha Isaya
10 Yeremia: kitabu cha Yeremia
11. Yoeli: kitabu cha Yoeli
12. Yona: kitabu cha Yona
13. Yoshua: kitabu cha Yoshua
14. Malaki: kitabu cha Malaki
15. Mika: kitabu cha Mika
16. Mordekai: kitabu cha Esta
17. Musa: vitabu vya Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Kumbukumbu la Torati, Hesabu, Ayubu na Zaburi namba 90.
18. Nathani: vitabu vya 1Samweli na 2Samweli (baadhi ya sehemu)
19. Gadi: vitabu vya 1Samweli na 2Samweli (baadhi ya sehemu)
20. Nahumu: kitabu cha Nahumu
21. Nehemia: kitabu cha Nehemia
22: Obadia: kitabu cha Obadia
23. Samweli: kitabu cha Samweli (baadhi ya sehemu)
24. Sulemani: vitabu vya Mithali, Mhubiri na Wimbo Ulio Bora
25. Sefania: kitabu cha Sefania
26. Zekaria: kitabu cha Zekaria
27. Wana wa Kora: vitabu vya Zaburi 42, Zaburi 44-49, Zaburi 84-85, na Zaburi 87-88
28. Asafu: vitabu vya Zaburi 50, na Zaburi 73-83
29. Ethani: kitabu cha Zaburi 89 (baadhi ya sehemu)
30. Heman: kitabu cha Zaburi 89 (baadhi ya sehemu)
31. Aguri: kitabu cha Mithali (namba 30)
32. Lemueli: kitabu cha Mithali (namba 31)
VITABU VYA AGANO JIPYA
1. Mathayo: kitabu cha Mathayo
2. Marko: kitabu cha Marko
3. Luka: vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume
4. Yohana: vitabu vya Yohana, 1Yohana, 2Yohana na Ufunuo
5. Yakobo: kitabu cha Yakobo
6. Yuda: kitabu cha Yuda
7. Paulo: vitabu vya Warumi, 1Wakorintho, 2Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Waebrania, Wakolosai, Wafilipi, 1Wathesalonike, 2Wathesalonike, 1Timotheo, 2Timotheo, Tito na Filemoni.
8. Petro: vitabu vya 1Petro na 2Petro
Kwa nini waandishi wapo zaidi ya 40 na si 40 kamili? Ni kwa sababu katika Agano la Kale, biblia pia imewataja wana wa Kora, ambao haijulikani walikuwa ni wangapi, lakini walikuwa zaidi ya mmoja. Pia, kuna vitabu 48 katika Zaburi, ambavyo waandishi wake hawajulikani.
Kwa ujumla, Biblia iliandikwa na takriban watu 40 katika kipindi cha miaka 1,600.
Ni kitabu cha Mungu kilichoandikwa na WATU, kwa uvuvio wa ROHO MTAKATIFU (2Timotheo 3:16).
Kwa kweli, Biblia ni maktaba ndogo yenye vitabu 66. Ina vitabu 39 vya Maandiko ya Kiebrania, ambavyo kwa kawaida huitwa Agano la Kale, na vitabu 27 vya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, ambavyo huitwa Agano Jipya, jumla vitabu 66.