Watu 396 wafa Dar kwa ajali za pikipiki

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170


396 wafa Dar kwa ajali za pikipiki


na Zawadi Chogogwe

Source: Tan Daima

WATU 396 wameripotiwa kufa katika ajali 2,856 zilizohusisha pikipiki 3,659 zilizotokea katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, jana ofisini kwake Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mohamed Mpinga, alisema ajali hizo pia zilisababisha majeruhi 2,418.


Alisema ajali nyingi zinazotokea hivyo kusababisha vifo vya watu hao hutokana na madereva wengi hasa wa pikipiki kuwa wakaidi kuvaa kofia ngumu.


“Madereva wengi wa pikipiki wanaosababisha ajali hawana utamaduni wa kuvaa kofia; hawana leseni na elimu yao ni duni pia wengine hawajapata mafunzo na kushindwa kufuata sheria za barabarani,” alisema Mpinga.


Alikiri kuwa kuna ongezeko la pikipiki hapa nchini kuwa kubwa jambo ambalo linawafanya wasimamizi wa sheria barabarani kushindwa kuwashurutisha na kuwakamata.


Alisema wameanzisha kampeni ya utii wa sheria barabarani bila kuwashurutisha madereva hao na kuwapa adhabu ya papo kwa papo au kuwapeleka mahakamani kwa wale a

My Take:

Wakuu hizi data ni kweli au zimepikwa???????? Kama ni kweli basi something is very wrong in our society. Vifo hivyo ni vingi mno katika miezi 6 tena kwa Dar pekee! Najiuliza

1. Je ni hatua gani zimechukuliwa? Kwa data hizo kuna haja hata ikiwezekana kupiga marufuku daladala-pikipiki mpaka hapo utaratibu na proper regulations zitakapotekelezwa

2. Nini hasa chanzo cha ajali hizo?

3. Je watanzania na serikali yao are they somehow shocked kuona such a huge no. of human lives?

4. Hivi human life ya a common Tanzanian inajaliwa kweli?

Kwa Marekani a loss of human life is averaged at a cost of $6 million (Soma hapa), the only index I found available so far with regard to monetary value of human life. Ukichukulia hiyo hesabu ni sawa na 6mn x 396 = $2 ,376, 000, 000.00 karibu nusu ya bajeti yetu.
 
Inasikisha sana! na kila siku ajali zinazidi kuongezeka, kila mwaka tutakuwa tunapoteza zaidi watu 1000
 
Back
Top Bottom