Watu 3000 kuhamishwa Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 3000 kuhamishwa Mbagala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Sep 13, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]WAKAZI zaidi ya 3,000 wa Bugudadi, Mbagala katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wako mbioni kuondolewa kwenye maeneo wanayoishi mabondeni ili kupisha uhakiki na tathimini ya nyumba zao.[/h]Tayari nyumba zao ziwekewa alama ya ‘X’ huku kukiwa hakuna taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi kuhusu hatua hiyo.
  Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Diwani wa Mbagala, Agrey Kayombo na wananchi.
  Wananchi hao walifikisha kilio chao kwa diwani kuwa wamekumbwa na wasiwasi baada ya nyumba zao kuwekwa alama hiyo huku kukiwa hakuna taarifa za kujitosheleza kutoka kwa viongozi wa wilaya yao.

  “Hii hali imetushtua sana ukichukulia miongoni mwetu tumekuwa tukilipa kodi ya majengo, hii inatufanya tusite kuendelea kulipa kodi kwa sababu hatutakiwi tena katika eneo hili,” alisema mmoja wananchi hao.
  Kwa upande wake Kayombo alisema tangazo hilo ni halali na ni agizo la Mkuu wa Mkoa la kuzitaka Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha zinawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo hatarishi ya mabondeni, ili kuwaepusha na majanga kama yaliyotokea Jangwani Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa mwaka jana

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kazi ipo mwaka huu.
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,339
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Serikali legelege hii...ramani za miji wanazo halafu hazifuatiliwi mpaka watu wajenge ndio wanakurupuka...
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  wao ndio wanaiweka ccm madarakani, wacha iwafundishe kufikiri, jawabu wanalo wao
   
 5. m

  makeda JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mh kujenga dar ni kujitafutia maradhi ya moyo,mh.sjui mikoani hali iko ivi ivi
   
 6. s

  shadhuly Senior Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo chadema wakitawala wataachwa wajenge mabondeni?

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Hapana, wawaondoe kwa kuwalipa stahili yao. Historia inaonyesha serikali ya CCM imekuwa ikiwalalia wananchi. Wasijenge mabondeni waondoe basi kwa staha,, utu na heshima, Mwambani Tang mradi wa bandari extension, watu walionewa sana mpaka leo wanalia with negligible compensation
   
 8. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  wawalipe kwa lipi? yani mtu kavunja sheria halafu tena ukamlipe? kuwaondoa kwa staha kivipi zaidi ya hivyo wameshaaambiwa wahame na nyumba zimeshawekwa X sasa staha gani zaidi ya hiyo tena? Piga tu tinga tinga kesho watafikiria mara mbili kujenga pasiporuhusiwa!

   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Rafiki hizi sehemu zilikuwa wazi tangu zamani bila mamlaka yoyote. They wwere open to everybody to acquire. Ziliumbwa na Mungu kabla ya mwanadamu kuziwekea sheria, Walipoingia hawa hapakuwa na sheria ya kuwazuia kuwa pale, hivyo ukiwaingilia uwalipe.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani apo ndo huwa nachoka ivi hao watu ambao mnawaondoa mabondeni na izi mvua ambazo kila kukicha zazidi kupunguankwa uchafuzi wa mazingira mtawalipa fedha sahikimkweli ili ukonwaendako wakajenge nyumba nasio kukaa kwenye mahema au kutelekezwa!
   
 11. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Duh! Ugumu wa maisha uko hapo sasa! manake mafuriko yakija na kuwasomba tunarudi kulalamikia mamlaka haijali watu wake!
   
 12. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  As if the only solution ni kuvunja nyumba ... Kwa nini wasitumie hizo nguvu & hiyo pesa kusafisha hayo mabonde maji yapite? Mto Msimbaze au Mto Mbezi ukusafishwa na kujengewa kuta vizuri tutasahau mafuriko.
   
 13. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  daaah,haya kapten
   
Loading...