Watu 3 wamefariki dunia katika ajali mbaya mkoani Mbeya

Watu 3 wamefariki dunia katika ajali mbaya mkoani Mbeya

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,335
watu 3 wamefariki dunia papo hapo baada ya malori 2 ya mizigo moja likitokea DAR na lingine ZAMBIA kugongana uso kwa uso na baadaye kuwaka moto eneo la mlima Kinyara mkoani mbeya.

source ITV Breaking News
 
Ilikuwa n balaa na ajal mbaya sn msongamano wa kufa mtu nimeliona hilo wkt nikiwa ndan ya gar.may their soul rest in peace
 
Kusababisha vifo.
Mnamo tarehe 26.09.2013 majira ya saa
06:45hrs huko katika mteremko wa
pipe line inyala barabara ya mbeya/
iringa wilaya ya mbeya vijijini mkoa
wa mbeya. Gari t.605 axx /t.480 cax
aina ya scania lori likitokea nchini
zambia kuelekea dar – es salaam
likiendeshwa na dereva wilson
macha, akiwa na tingo wake juma s/o
salehe wote wakazi wa dsm [ambao
katika ajali hiyo wote wamefariki
dunia] liligonga kwa nyuma gari
t.548 bly/ t.974 bvn aina ya scania
lori lililokuwa likiendeshwa na
dereva samwel aron , miaka 30,
mbena, mkazi wa sinza, kisha gari
hilo lililigonga gari t.876 bkv/t.465
bqu aina ya iveco lori ambalo
lilikuwa limeegeshwa pembeni ya
barabara likiwa limeharibika,
lililokuwa likiendeshwa na dereva
samwel kasusu , miaka 37, mjita, mkazi
wa gongo la mboto dsm.
Aidha gari hilo t.605 axx /t.480 cax
likiwa limepoteza mwelekeo
liligongana uso kwa uso na gari
t.255 akv/t.272 cdz aina ya scania
lori lililokuwa likitokea dsm
kuelekea mbeya mjini ambalo lilikuwa
linaendeshwa na dereva sixtus s/o
kapinga, miaka 35,mngoni, mkazi wa
dsm ambaye alifariki dunia papo hapo
na mwili wake kuteketea kwa
kuungua moto.
Katika ajali hiyo magari mawili t.605
axx /t.480 cax na t.255 akv/t.272 cdz
yote yameungua vichwa na kuteketea
na gari t.548 bly/ t.974 bvn liliungua
kidogo sehemu ya kichwa upande wa
kulia.
Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa
gari t.605 axx /t.480 cax .
Moto ulizimwa kwa ushirikiano kati
ya kikosi cha zima moto na uokoaji
kwa kushirikiana na jeshi la polisi na
wananchi.
Miili ya marehemu wilson macha na
juma salehe imehifadhiwa hospitali
ya rufaa mbeya. Jitihada za kuutoa
katika gari mwili wa marehemu
sixtus s/o kapinga pamoja na kutoa
magari eneo la tukio zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya
kamishna msaidizi wa polisi diwani
athumani anatoa wito kwa madereva
kuwa makini wanapotumia vyombo
vya moto kwa kuzingatia sheria na
alama za usalama barabarani ili
kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
 
Crying for all but my bro sixtus Kapinga umeenda Leo kaungua jamani kabisa rip bro ImageUploadedByJamiiForums1380227992.496473.jpg
 
huyo mwana alikuwa ni zaidi ya rafiki

tena bado kijana nguvu ya taifa. pole sana mkuu yote maisha sisi ni wapita njia tu .
cha muhimu kumuomba mungu sababu nasikia barabarani kuna mapepo pia
 
Back
Top Bottom