Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,602
- 22,707
Karibu watu 100 waliokuwa katika sherehe za harusi wameangukiwa na ukuta na paa baada ya hoteli kubomoka nchini Peru
Hoteli yabomoka 13 wafariki
Zaidi ya watu 13 wamepoteza maisha katika kijiji cha Tamburco nchini Peru, wakiwa katika sherehe za harusi baada ya ukuta na paa la hoteli kubomoka.
Taasisi ya ulinzi wa jamii nchini Peru (INDECI) imetoa taarifa ya kwanza inayofahamisha kwamba katika jimbo la Apurimac mjini Abancay kijiji cha Tamburco watu karibu 100 waliohudhuria sherehe za harusi wameangukiwa na ukuta na paa la hoteli. Kujtokana na ajali hiyo 13 wamepoteza maisha huku 30 wakiwa wamejeruhiwa.
Kiongozi wa INDECI Jorge Chavez alisema tukio hilo lililotokea usiku inaweza kuwa limechangiwa na mvua kubwa zinazonyesha eneo hilo pamoja na miundombinu mibovu.
Timu za uokoaji zinaendelea na kazi ya kuchimbua vifusi katika kutafuta watu ambao wanaweza kuwa bado wamefukiwa vifusi hivyo inaendelea.
Chanzo: TRT Swahili