Watu 12 wafariki kutokana na foleni ya magari

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
151224061923_delhi_traffic_jam_640x360_afp_nocredit.jpg

Wengi walikuwa wakisafiri baada ya mwisho wa mfungo wa Ramadhan
Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha.

Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu. Watu wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java.

Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea. Maafisa wa uchukuzi nchini Indonesia wanasema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku tatu.

Vyombo vya habari nchini Indonesia vinasema wengi wa waliofariki ni wazee ambao walikwama ndani ya magari chini ya joto kali. Mtoto mmoja mchanga alifariki kutokana na kinachodhaniwa kuwa ni kupumua hewa chafu iliyojaa moshi wa magari.

Chanzo: BBC
 
Asee kifo popote unaeza ukafa huku unasoma hata gazeti
 
ndio maana kuna umuhimu wa boda boda hapo ilikuwa unazima gari unachukua boda mpaka dukani unanunua maji lita zako tano unarudishwa kwenye gari yako unaendelea na foleni yako yaani ni mwendo wa "ecosytem" kwenye vyombo vya usafiri pamoja na madereva........eti huku mnasema zisiingie mjini mtakuja kufa kama hao....
 
Back
Top Bottom