Mkuu kibao cha gharama kikigeuka inakuwaje?
atakaebeba gharama kubwa malezi ndo aamue
usiseme tuanze kuzaa now na tuzae watoto 16 wakati
wewe unamtegemea mwenzio kwa pesa za matunzo
Na malezi ni pesa tu?
Wadau. Hivi mnapokuwa mmeshaoana, ni nani anayetakiwa apange kwamba 'huu ni wakati wa kupata mtoto'? Ni mume, ni mke, baba/mama mkwe au ni ile ghafla tu kitoto kinatokea!?
Kuna rafiki yangu ametengana na mke wake kwa sababu ya mtoto, kwamba jamaa hakuwa anataka mtoto mapema. Na isitoshe walikuwa hawakai pamoja kwa sababu ya kazi. Jamaa yupo Iringa mke Dar.
Wakati wa usulihishi wa swala lao, jamaa akasema "mke wangu unajua kabisa nilikuambia tusizae mapema, sasa imekuwaje?" Alichojibu mke ndio kilichonifanya niulize mauzoefu hapa. Alijibu "wewe unadhani tulioana ili tupike makande?". Hapo jazba zikaanza kikao kikavunjika, na hadi leo wametengana.
Wote wanatakiwa kukubaliana mda gani wazae.
Makubaliano ndio kila kitu hapa!
Ikitokea ndoa kwa bahati mbaya ie negligence is included! NO BLAMES! but mmoja wao usipotii makubaliano willingly/by malice/intentionaly, can't blame ze impacts upon him/her!
mkishaoana kuna watoto wa kupanga, na watoto wanaojileta wenyewe.....
kwa wale wa kupanga mi naona ni vizuri wote wawili mkakubaliana. ila sasa kuna wale ambao mama umekaa zako unashangaa siku zinayoyoma tu hakuna dalili za usichana...... hapo sasa hakuna wa kumlaumu mwenzie
Ila mkuu unakubali kuwa maamuzi yapo kwenye mkono wa mwanamke? Hata kama unajua mzunguko wake, inaweza ikatokea dharura ramani ikageuka..ukapewa, na ukapiga vizuri ukijua hakinasi kumbe ndio tayari.