Watoto wetu wanaposhindwa kufaulu

Watoto wetu wanaposhindwa kufaulu

JUSTIN MPOTWA

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
16
Reaction score
11
Ifike wakati sasa tusilaumiane kwa kuwa jamii nzima inahusika. mpaka sasa tumesikia matokeo ya mitihani ya taifa miwili; wa darasa la saba na wa kidato cha pili lakini kote kuna tisha!

Nayagawanya matatizo ya kufeli kwa wanafunzi katika makundi makubwa yafuatayo ya kimalezi:

1. MALEZI YA WATOTO KATIKA UMRI KATI YA MIAKA 0-5
2. MALEZI YA WATOTO KATIKA UMRI KATI YA MIAKA 5-UMRI WA BALEHE
3. MALEZI YA VIJANA KATIKA UMRI KATI YA UMRI WA BALEHE-UMRI WA KUCHAGUA FANI ZA MAISHA
4. MALEZI YA VIJANA KATIKA KUZIKUZA FANI ZAO

Tunatambua kuwa asilimia zaidi ya 75 ya uwezo wa kufikiria wa mwanadamu huwa inategemea malezi aliyoyapata akiwa na umri chini ya miaka mitano (5) na mara nyingi kwetu Tanzania ni umri ambao watoto huwa chini ya uangalizi wa wazazi/walezi.

Pia tunatambua kuwa asilimia zaidi ya 75 ya kuishi kwetu inategemea namna jamii yetu inavyoishi na jamii ndiyo yenye jukumu kubwa ya kutusaidia kuishi kwa kadri ya maadili ya kijamii na mara nyingi hapa kwetu Tanzania zaidi ya asilimia 75 hiyo tunaitumia tukiwa shuleni.

Maswali ya kujiuliza:

Je, tuwalaumu wazazi/walezi waliotulea wakati tukiwa na umri chini ya miaka mitano(5) kwa maana wao ndio waliokuwa na dhamana ya kukuza uwezo wetu wa kufikiria!

Je tuwalaumu wanajamii amabao kwao tumetumia zaidi ya asilimia 75 ya maisha yetu tukiwa na umri baada ya miaka mitano?

Kwa kuwa kiasi kikubwa asilimia fulani ya asilimia 75 ya maisha yetu inatumiwa tukiwa shuleni, Je, tuilaumu serikali ambayo haina mfumo mzuri wa kielimu?

MTAZAMO WANGU
Kila mmoja achukuea hatua! Jambo moja kwa serikali ni kuhakikisha inaunda falsafa ya elimu itakayo saidia kuondoa matatizo ya kimalezi kwa kadri ya makundi niliyoainisha pale awali.
 
Naunga mkono hoja yako.kusema ukweli wazazi nao wanachangia katika hili mihangaiko ya maisha imekuwa mingi hivyo wazazi wanakuwa na mchango mdogo wa malezi kwa watoto wao wanawaachia wasaidizi wa kazi.nawasihi wazazi wawe wanafuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni mpaka nyumbani nafikiri hali itabadilika
 
Well said but if you want a thing done well, do it for yourself....
 
Well said but if you want a thing done well, do it for yourself....
absolutely. huwa nashangaa watu wanaolalamika daily, wakati wao hawajitumi
  1. jirani anaonesha muvi za xxx, badala ya kukemea; analalamika 'serilaki haichukui hatua...'
  2. watu wanaharibu vyanzo vya maji, hawaundi mgambo kuzuia; wanalalamika 'serikali haichukui hatua....'
  3. mwanae anakutana na marafiki wabaya, hamkanyi; analalamika 'vijana siku hizi wameharibika..'
  4. nk
 
Back
Top Bottom