Watoto wangu wananifilisi

Ni kweli. Ndio kosa tunalofanya siku hizi. Mwisho wa siku tunalea watoto wanaofikiria the whole world rotates around their feet. Watajikuta badala ya kufanya kazi kwa bidii wapate watakacho wanaishia kulalwa na bosi ili afanye short cut.

Sisi tulikuwa hatuchapwi, unapewa adhabu yenye manufaa. Utamsaida dada kuosha vyombo wiki nzima. Ilikuwa motivation kubwa ya kutokukosea, lakini pia kujifunza kazi.
 
Wapeleke boarding schools watajifunza life tofauti ya kutokudekezwa
 
Bro jaribu kuwajenga watoto wako waweze kudhibit tamaa zao, sio kila wanachotaka lazima wapate..wape tu vitu vyenye umuhimu...

Pia jipe muda wa kuwa unaongea nao na kuwafundisha kuwa maisha ni shida na raha...na pia wajue kutambua tofauti ya mahitaji yenye umuhimu na yale ya ziada...Kuna leo na kesho Bro.

Vile vile nakushauri tu hasa kwa huyo mtoto wa kiume usimzoweshe maisha ya kike hayo ya kula kula hovyo hasa ma chips...

LEA WATOTO WAKO UNAVYOHISI INAPASWA WAKUE KIAFYA NA KIMAADILI, WEWE NI MLEZI, KIONGOZI NA MWALIMU KWAO!!!
 

WASIPOKULA VYAKO WALE VYA NANI?
 
Hao wa kiume soon utawaona Take One ya Cloud TV na seneta wao Kaoge.
 
Wewe wadekeze tu, utavuna unachopanda.
 
Sasa unataka wampige nani mizinga?

Sijui wengine lakini mimi ikija kwa Kisura huwa nafanya kufuru.

Chochote atakacho anapata tu.

Ndo wajibu wangu huo na kamwe siwezi kulalamika.

Na furaha yake ndo faraja yangu.
Wafundishe kujitegemea na kusave pesa.
 
Inaoneka unauzoefu na hii ki2,ushauri mzuri
 
Namfundisha zaidi ya hayo!

Life skills siyo kujitegemea na kusevu pesa tu.
Kama wanafundishwa zaidi ya hayo, katika hayo ya zaidi, kuwa mambo ya dini? Je wanafanya ibada kanisani au msikitini?
 
Kama wanafundishwa zaidi ya hayo, katika hayo ya zaidi, kuwa mambo ya dini? Je wanafanya ibada kanisani au msikitini?

1] Aliyepo ni mmoja tu. Sina zaidi.

2] Suala la imani ya dini ni uamuzi wake. Mimi hilo kwangu halina umuhimu wala maana yoyote ile.
 
Kama unamudu kuwahudumia hakuna ubaya watoto wako wakifaidi pesa zako ila usiwazoeze mazingira kuwa pesa ndio kila kitu maana utawaharibu. Pamoja na kuwapa pesa,wafundishe stadi za maisha ili wayajue maisha black and white na sio kuishi katika bubble. Wasafirishe kijijini wakaishi na wazee,wajue wengine wanaishi vipi,wafundishe kusimamia biashara, kufanya kazi za nyumbani na hata kusaidia jamii iliyowazunguka. Wapatie majukumu yenye malengo fulani ya kufikiwa, wafundishe ufundi wa kuunda au kurekebisha vitu fulani vya nyumbani au vyombo vyako vya usafiri ili wawe na ujuzi fulani wa kimaisha,sio unakuwa na mtoto yuko form four hata kubadili tairi hawezi, kurekebisha kitasa hawezi na kupika ndio kabisa. Usiwalee watoto wakajiona wako special sana na tofauti na wanadamu wengine na utafurahi kuwa nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…