Teleskopu
JF-Expert Member
- May 5, 2017
- 703
- 768
Kwa mara ya mwisho serikali ilinunua vitabu kwa shule za msingi wakati pesa za rada ziliporudishwa serikalini.
Miaka inaenda, watoto wanazidi kusogea madarasa bila kuwapo vitabu.
Serikali imejaribu kuandika vitabu kupitia TIE imeshindwa (so far).
Shule nazo haziwezi kunua vitabu kwa sababu haieleweki iwapo serikali itarudia mtaala wa zamani au huu unaoitwa mpya. Hakuna matamko ya wazi na thabiti.
Siku zinaenda na watoto wanapanda madarasa.
Na hawa watoto ndio taifa lenyewe.
Itakuwaje kama siku moja nchi itasema: "Hatutaandikisha watoto wa darasa la kwanza kwa miaka mitatu kuanzia sasa"?
Je, kutonunua vitabu kwa miaka kadhaa kuna tofauti gani na kufanya uamuzi kama huo?
Siku zinaendana watoto wanahama madarasa.
Waliokuwa darasa la tatu, sasa ni la saba - bila vitabu.
Nini maana ya mambo haya?