Kuna tabia naona inazidi kushika kasi kwenye Mabasi ya Mwendokasi nayo si nyingine ni ya wazazi kuwaacha watoto wadogo ambao ni wanafunzi umri kati ya miaka 5 hadi 6 kusafiri peke yao bila uangalizi kwenda na kurudi shuleni.
Kwa wale watumiaji wa usafiri huu mtakuwa mashahidi watoto hawa ukweli huwa wanasikitisha sijui wazazi wao wanafikiria nini?
Wazazi wenzangu chondechonde kama huna uwezo wa kulipia "school bus" bora watoto watafutie shule za karibu, haya mabasi kuna wakati yanakuwa yamesheheni abiria, na watoto hawa ni wadogo huwa wanahangaika kutafuta hewa/nafasi.