The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,455
- 12,236
PYGMY MARMOSETS ni jamii ya nyani wadogo wanaopatikana hasa katika ukanda wa tropic kwa umoja wao huitwa Cebuella.
Jamii hii ni wakazi wa ukanda wa amazon huko America ya kusini iwemo Brazil, Colombia, Ecuador, Peru na Bolivia. Nyani hawa wanatambulika kama nyani wadogo zaidi duniani, wakiwa na uzito wa gramu 100 tu.
Pygmy Marmoset huishi katika mfumo wa kimakundi (familia); ya wanafamilia kati ya wawili hadi tisa. Ikiwemo dume la kuu, majike, na mpaka watoto 4 au zaidi.
Kwa ukawaida ukubwa wa kundi huwa na washiriki 6. Majike huzaa watoto mapacha mara moja au mbili kwa mwaka ambako matunzo ya watoto hao ushirikisha wazazi pamoja na wanafamilia wengine kwa pamoja. Kwani utunzaji wa watoto hawa ni mgumu kutokana na hali ya kimazingira na maumbile yao.
Nyani hawa chakula chao kikuu ni utomvu wa miti na wadudu; sana sana vipepeo. Huku maadui wa kubwa wa jamii hii ya nyani ni ndege wawindaji, Paka wadogo, pamoja na nyoka.
Jamii zote za pygmy marmosets zimeorodheshwa kati ya jamii za wanyama walio hatarini kutoweka kulingana na shirika la kimataifa la The International Union for Conservation of Nature (IUCN):- Red List of Threatened Species.