Watoto wa mitaani na wanavyotumika

Watoto wa mitaani na wanavyotumika

Kwanza hongera sana kwa roho yako nzuri kwa wema uliomtendea huyo mtoto....
Je,huyo mtoto yuko wapi sasa hivi?

Mungu Akubariki Kwa Moyo Wako...Ila Ukirudi Usiste Kujibu Maswali Ya Wenzangu Hapo Juu Kwan Ninashauku Ya Kujua Alipo Huyo Mtoto

mkuu huyu mtoto mpaka sasa nipo naye nyumbani na nimeshaenda kutoa taarifa polisi suala lake linashughulikiwa pamoja na kutafuta mzazi wa huyu mtoto.
 
Swali la kizushi, why mtoto alitoroka nyumbani kwako na ulipomfuata akagoma kurudi.? Na kwa mujibu wa maelezo akakubali alipoona wahuni wanamfuata.?
mkuu huyu mtoto alitoroka nyumbani kutokana na mazingira, kumbuka huyu mtoto maisha yake ni kuzunguuka tu mitaani. alipofika nyumbani na kuona mazingira yako tofauti kidogo ndio alipotoroka. halafu anaonesha kabisa kutokana na matendo aliyofanyiwa uaminifu kwa watu wanaomzunguka umepungua kwa kiasi kikubwa sana. ila sio mbaya tumempeleka kwa psychologist hali yake inaweza kurudi kama kawaida.
 
Hao watoto wadogo wa Ubungo wanalawitiwa Sana'a....Wanalawitiwa wao kwa wao au na Yale majamaa majitu mazima pale Ubungo.
Niliwahi kujifanya na Mimi ni teja na kibaka kwa siku kadhaa pale Ubungo...ili tu nijue hali iliyopa pale,Kiukweli kuna mengi sana yanayoendelea kwa wale watoto.
Kwa kweli wale watoto wengi kula yao inategemea kulawitiwa...Lakini Waziri husika yupo Saloon kujikoboa ili vijana wadogo wamapigie mruzi

inasikitisha sana mkuu! wanaohusika na mambo haya kama hawaoni ! hawana habari kabisa
 
hongera sana kwa moyo wa huruma ,ushauri naoutoa kwa wanaumewenzangu walio oa mke wa pili baada ya kuachika au kufiwa na mke wa kwanza wasikubali mashitaka yeyote kutoka kwa mama wa kambo ,kama kweli unawapenda wanao, ambao ndiyo ndugu zako, mke atabaki kuwa mke siyo ndugu ukiachana naye basi tena ,mfano umetoka kazini saa nne usiku unaambiwa kwamba wanao leo wamenitukana bila kufanya utafiti unawakurupusha watoto ambao wamekwisha lala na kuanza kuwapiga haifai
 
Inasikitisha sana na hongera bw mutant kwa roho ya imani
 
Back
Top Bottom