Mimi kama mdau wa Kifipa nasema kuwa wasichana wa Kifipa ni wasichana wanaojiheshimu na wanaojua kuzitunza ndoa zao,kama unataka kupigiwa goti mpaka chini karibu kwetu Ufipani, kama unataka msichana ambae hata hakosi kwenye misa ya parokiani na nyumba kwa nyumba njoo huku kwetu Ufipani, kama unataka msichana mvumilivu ambae unaweza ukasafiri kwa mwaka mzima ukamkuta salama njoo kwetu Ufipani. Kasoro yetu bwana ni kwamba sie ni wanywaji wazuri wa pombe ya kienyeji aina ya Sute iwe kwa mama,baba na mtoto wafipa tunapiga pombe kwa kwenda mbele