Watoto wa Cleopa Msuya watinga mahakamani kugombea mali

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
8,084
Reaction score
20,225
Watoto watatu wa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Cleopa Msuya, wameingia katika mvutano wa kisheria kuhusu usimamizi wa mirathi ya baba yao, huku Mahakama Kuu ikifungua njia ya kusikilizwa kwa maombi ya kulinda mali za marehemu.

Katika uamuzi uliotolewa Oktoba 13, 2026, Jaji Sara Mwaipopo wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Temeke, alitupilia mbali mapingamizi matano kati ya sita yaliyowasilishwa na John Msuya na Naanjela Msuya dhidi ya maombi ya Job Msuya, aliyekuwa akiomba amri za muda za kuhifadhi mali za mirathi.

Job, kupitia Wakili Albert Lema, aliiomba mahakama kuingilia kati akidai wasimamizi wenzake walikuwa wakifanya maamuzi kuhusu mali za marehemu bila ridhaa ya pamoja. Pia alieleza wasiwasi kuhusu nyumba iliyopo Upanga, akidai ilikuwa katika hatari ya kuuzwa kwa bei ya chini au kukodishwa kwa masharti yasiyozingatia masilahi ya mirathi.

Wasimamizi hao waliwasilisha mapingamizi sita wakidai maombi hayo hayakuwa na msingi wa kisheria, yalikuwa yamewasilishwa mapema kabla ya kukamilika kwa orodha ya mali, na kwamba kulikuwa na shauri jingine lenye hoja zinazofanana. Pia walipinga hati ya kiapo ya Job na kudai maombi yalikuwa yamepitwa na muda wa kisheria.

Hata hivyo, Jaji Mwaipopo alieleza kuwa mahakama ina mamlaka ya kutoa amri za kuhifadhi na kulinda mali za mirathi hata kabla ya kuwasilishwa kwa orodha ya mali, hasa pale kunapokuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa mali kuuzwa au kuharibiwa. Pia alibaini shauri jingine lililotajwa na wajibu maombi lilikuwa tayari limefutwa.

Jaji alikubali kwa sehemu pingamizi kuhusu hati ya kiapo, akiamuru aya za 7, 20, 21, 23, 24, 25 na 26 zifutwe kwa kuwa zilikuwa na kauli za imani, maoni na hoja za kisheria ambazo hazikupaswa kuwasilishwa kwa namna hiyo. Hata hivyo, alikataa ombi la kutupilia mbali hati nzima, akisema kasoro katika baadhi ya aya hazibatilishi hati yote.
 
Watoto watatu wa aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais wa Tanzania Cleopa Msuya wameingia katika mvutano wa kisheria kuhusu usimamizi wa Mirathi ya baba yao .
Kisa hiki ni moja ya visa vingi vinavyotokea mara baada ya mmiliki wa mali anapofariki watoto au ndugu hufarakana sana na kupelekana mahakamani na wengine kufikia hatua ya kuuwana.

Source. Gazeti la mwananchi
mali za hawa viongozi ingetakiwa sisi wote tushiriki kwenye mirathi maana ni keki yetu ya Taifa.🤣🤣
 
Watoto watatu wa aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais wa Tanzania Cleopa Msuya wameingia katika mvutano wa kisheria kuhusu usimamizi wa Mirathi ya baba yao .
Kisa hiki ni moja ya visa vingi vinavyotokea mara baada ya mmiliki wa mali anapofariki watoto au ndugu hufarakana sana na kupelekana mahakamani na wengine kufikia hatua ya kuuwana.

Source. Gazeti la mwananchi
Nyingi ya mali za namna hii huwa ni zile zilizopatikana kwa namna zisizoeleweka
 
Watoto watatu wa aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais wa Tanzania Cleopa Msuya wameingia katika mvutano wa kisheria kuhusu usimamizi wa Mirathi ya baba yao .
Kisa hiki ni moja ya visa vingi vinavyotokea mara baada ya mmiliki wa mali anapofariki watoto au ndugu hufarakana sana na kupelekana mahakamani na wengine kufikia hatua ya kuuwana.

Source. Gazeti la mwananchi
ok.🐒
 
Africa uninafsi unatumaliza. Ndio maana hatutengenezi matajiri. Baba kakusanya, mitoto kwa ubinafsi inakuja kutawanya. Hapo utasikia wanajisemea, tugawane kila mtu afe na chake 😀😀😀😀
 
Mtu yeyote msomi / familia ya wasomi haya mambo kugombea Mali za mzee utasikia kwa familia za mafukara wa AKILI (maskini wa akili) hakuna UMASKINI mbaya kama UMASKINI wa MAARIFA

NB. SISI MZEE ALITUPA ELIMU TENA AKASEMA HATA TUSIPO MSAIDIA KWA CHOCHOTE ATLEAST TUWEZE KUJIMUDU KABLA HAJAFA ALIHAKIKISHA MALI KAZIGAWA KWA ALIO WAPENDA FULL STOP

KILA SIKU HUWA NAZUNGUMZA NA WEWE KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NAMISS CALL ZAKO

KILA LEGACY YAKO IPO VYEMA WALA HATUJAGOMBANIA CHOCHOTE ZAIDI YA KUWA WAMOJA NA KUKUENZI DAIMA

ATLEAST MIMI NA NDUGU ZANGU TULIKUA NA BABA... BABA AMBAE NIKIJARIBU KUWA BABA BORA KULIKO YEYE VIATU VINAPWAYA PUMZIKA MZEE WANGU
 
Ilitakiwa kabla ya kufariki kila kijana apewe sehemu yake ya kusimamia.

Africa uninafsi unatumaliza. Ndio maana hatutengenezi matajiri. Baba kakusanya, mitoto kwa ubinafsi inakuja kutawanya. Hapo utasikia wanajisemea, tugawane kila mtu afe na chake 😀😀😀😀
Mkuu, nadhani hapa unapaswa kuangalia kwa kina kabla ya kuhukumu na kusema 'ubinafsi unatumaliza.' Naruhusiwa kuweka disclaimer hapa kwa sababu namfahamu binafsi mtoto wa kwanza wa Mzee Msuya, yaani George Msuya, na nimeshafanya naye kazi miaka ya huko nyuma. Nakuhakikishia kwa asilimia mia moja, hawa watoto wako tofauti sana na wale watoto wa viongozi wengine tunaowajua sisi ambao baba zao walishika madaraka makubwa kama ya huyu Mzee.
Hawa si watoto wa 'kuhongwa' magari, kuishi kwa uvivu, au kufuja mali wakitegemea jina la baba yao. Mzee Cleopa Msuya alisifika kwa kusomesha watoto wake na kuhakikisha kila mmoja anasimama kwa miguu yake kitaaluma na kuwa na maisha yake ya heshima:
  • George Msuya – Mtoto wa kwanza, ni Mhandisi (Engineer) mbobezi na mwenye weledi wa hali ya juu kwenye kazi zake.
  • Dr. John Msuya – Mtoto wa pili, ni Daktari wa Binadamu (Medical Doctor) mwenye taaluma yake ya heshima.
  • Dr. Joyce Msuya Mpanju – Mtaalamu wa masuala ya mazingira na microbiology, aliyefikia hadi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP na sasa ni Afisa Mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa Umoja wa Mataifa (UN).
  • Job Msuya – Naye pia ni Mhandisi (Engineer) anayejiheshimu.
  • Naanjela (Angela) Esther Msuya – Mtaalamu mbobezi wa ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA (IT Systems Audit).
    (Kumbuka mtoto mwingine, Geofrey Msuya, alitangulia mbele ya haki tangu mwaka 2005).
Mkuu, watu wenye akili hizi, wasomi wa kiwango hiki, na wenye kazi zao kubwa hawawezi kwenda mahakamani kwa 'ubinafsi wa njaa' au 'kutawanya mali'.
Kisheria na kiungwana, kwenda mahakamani kupinga usimamizi wa mirathi sio ugomvi wala sio uharibifu; bali ni kutafuta tafsiri sahihi ya kisheria na kulinda mali zisipotee. Kwenye shauri hili la sasa, Job Msuya alienda mahakamani kuomba amri ya kulinda mali (kama vile nyumba ya Upanga) kwa sababu aliona wasimamizi wenzake wanafanya maamuzi bila ridhaa ya pamoja. Huku si kutawanya, bali ni kulinda mali isiyuzwe kienyeji au kwa bei ya chini chini chini ya kiwango.
Hawa watoto wana fedha na kazi zao. Wanachofanya sasa ni kusimamia taratibu zilizonyooka ili kile alichokiacha baba yao kibaki salama na kigawanywe kwa haki na uwazi. Wangekuwa hawajasoma au hawana akili, wangesafiri na mapanga au kurogana, lakini kwa sababu wameelimika, wametumia chombo halali cha sheria ambacho ni Mahakama Kuu.
Tusiwalaumu watoto kwa kutumia akili na sheria kulinda urithi wao!
 
Hapa ni engineer TU wanawaza wasiwe na njaa, nikuhakikishie TU huyo daktari, sijui mkaguzi wa tehama Wana njaa TU , na huenda bila mirathi ya baba yao wangekuwa sakala flani, ila nimependa mzee kafa na watu wanagombania Mali zako Ina maana ulitimiza wajibu wako duniani , mzee angejua angezaa watoto na wanawake tofauti tofauti isingeleta shida Kwa sababu kabla hujafa unandika mirathi sababu unajua ukifa TU Kuna ******* watauana kisa Mali zako
 
tanzagiza inabidi tufike mahali na tuamue aidha we are Christians or we are not Christians, hii vugu vugu haitufikishi popote zaidi ya mateso tu, kwa maana huku hatupo kote na kule pia kwenye mila mila siyo kote.

jamii Christians zote wana-define familia kama baba, mama na watoto na hilo ndilo jukumu la kwanza la wazazi ni kuangalia familia yao i.e watoto wao hao wengine wote ni kama kuna salio limebakia.

hivyo watu wa kwanza ni watoto na kaka, dada, baba, mama wa marehemu siyo wa kwanza hivyo watoto hawapaswi hata kujadili khs mali za wazazi wao na yoyote yule, ni moja kwa moja za kwao labda kama ni wao kwa wao lkn sijui ba mkubwa, shangazi hata hao pia wana familia zao waende huko …
 
Mkuu, nadhani hapa unapaswa kuangalia kwa kina kabla ya kuhukumu na kusema 'ubinafsi unatumaliza.' Naruhusiwa kuweka disclaimer hapa kwa sababu namfahamu binafsi mtoto wa kwanza wa Mzee Msuya, yaani George Msuya, na nimeshafanya naye kazi miaka ya huko nyuma. Nakuhakikishia kwa asilimia mia moja, hawa watoto wako tofauti sana na wale watoto wa viongozi wengine tunaowajua sisi ambao baba zao walishika madaraka makubwa kama ya huyu Mzee.
Hawa si watoto wa 'kuhongwa' magari, kuishi kwa uvivu, au kufuja mali wakitegemea jina la baba yao. Mzee Cleopa Msuya alisifika kwa kusomesha watoto wake na kuhakikisha kila mmoja anasimama kwa miguu yake kitaaluma na kuwa na maisha yake ya heshima:
  • George Msuya – Mtoto wa kwanza, ni Mhandisi (Engineer) mbobezi na mwenye weledi wa hali ya juu kwenye kazi zake.
  • Dr. John Msuya – Mtoto wa pili, ni Daktari wa Binadamu (Medical Doctor) mwenye taaluma yake ya heshima.
  • Dr. Joyce Msuya Mpanju – Mtaalamu wa masuala ya mazingira na microbiology, aliyefikia hadi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP na sasa ni Afisa Mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa Umoja wa Mataifa (UN).
  • Job Msuya – Naye pia ni Mhandisi (Engineer) anayejiheshimu.
  • Naanjela (Angela) Esther Msuya – Mtaalamu mbobezi wa ukaguzi wa mifumo ya TEHAMA (IT Systems Audit).
    (Kumbuka mtoto mwingine, Geofrey Msuya, alitangulia mbele ya haki tangu mwaka 2005).
Mkuu, watu wenye akili hizi, wasomi wa kiwango hiki, na wenye kazi zao kubwa hawawezi kwenda mahakamani kwa 'ubinafsi wa njaa' au 'kutawanya mali'.
Kisheria na kiungwana, kwenda mahakamani kupinga usimamizi wa mirathi sio ugomvi wala sio uharibifu; bali ni kutafuta tafsiri sahihi ya kisheria na kulinda mali zisipotee. Kwenye shauri hili la sasa, Job Msuya alienda mahakamani kuomba amri ya kulinda mali (kama vile nyumba ya Upanga) kwa sababu aliona wasimamizi wenzake wanafanya maamuzi bila ridhaa ya pamoja. Huku si kutawanya, bali ni kulinda mali isiyuzwe kienyeji au kwa bei ya chini chini chini ya kiwango.
Hawa watoto wana fedha na kazi zao. Wanachofanya sasa ni kusimamia taratibu zilizonyooka ili kile alichokiacha baba yao kibaki salama na kigawanywe kwa haki na uwazi. Wangekuwa hawajasoma au hawana akili, wangesafiri na mapanga au kurogana, lakini kwa sababu wameelimika, wametumia chombo halali cha sheria ambacho ni Mahakama Kuu.
Tusiwalaumu watoto kwa kutumia akili na sheria kulinda urithi wao!
Kama wameelimika, ni kitu gani kinacho wanyima mshikamano wa kutokusikilizana ili kufanya maamuzi ya busara ndani ya familia?

Hii kutoka nje kwenda mahakamani, ni kuonyesha dunia hakuna masikilizano.​
 
Back
Top Bottom