Watoto pacha wa Morogoro kutenganishwa

Watoto pacha wa Morogoro kutenganishwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Dar es Salaam.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhari amesema baada ya vipimo imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha watoto pacha walioungana.

Dk Bokhari ambaye amebobea katika upasuaji huo Afrika Mashariki, ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takribani wiki nzima.

"Vipimo vya damu vimeonyesha kila mtoto ana mfumo wake na hawana maambukizi ya aina yoyote, ugumu unakuja kwenye ini na moyo ambapo wanategemeana ila uwezekano wa kutenganishwa upo,"amesema Dk Bokhari.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo vyote vya damu.

Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali.

watt.jpeg


mwananchi
 
Inanikumbusha Gifted Hands. Watenganishwe kwa kweli ikibidi kama hapa hakuna technologia wapelekwe Marekani ama Germany.
 
Inanikumbusha Gifted Hands. Watenganishwe kwa kweli ikibidi kama hapa hakuna technologia wapelekwe Marekani ama Germany.

Pamoja na hilo,nasi katika ngazi ya familia tukazanie Elimu kwa watoto wetu kila mmoja kwa nafasi yake.Sanjari na hilo,tukazanie kuwekeza katika tafiti.Kuna tatizo kubwa linatengenezwa sasa na haya makanisa ya "Uponyaji" kuanza kupandikiza mbegu katika watoto ya kuamini nguvu ya miujiza iko ili kuhakikisha kila tatizo linamalizwa na miujiza hiyo.Mungu katika nyakati zetu anafanya kazi sana kupitia Sayansi na Tekinolojia.
 
Mungu awape wepesi....nilikuja mbio nilijua kina Consolata wale waliopata Division 2 waliomaliza form six
 
MUNGU tunaomba usaidie madaktari wetu wafanikiwe katika hili
 
Mungu awaongoze madaktari watakao wafanyia upasuaji watoto watoke salama inshaalah
 
"Vipimo vya damu vimeonyesha kila mtoto ana mfumo wake na hawana maambukizi ya aina yoyote, ugumu unakuja kwenye ini na moyo ambapo wanategemeana ila uwezekano wa kutenganishwa upo,"amesema Dk Bokhari.

Hapa daktari kanichanganya kama sio mwandishi kumnukuu vibaya. Anasema wana mifumo tofauti ya damu, halafu tena anasema wanategemeana kwenye moyo. Kwa elimu yangu ya biolojia, moyo ni kiungo muhimu katika mfumo wa damu. Halafu hajasema kama wana moyo mmoja au miwili.

Hapo tatizo kubwa inaonekana wana-share ini na moyo au watuambie kuwa kila mmoja ana kiungo chake lakini vimeungana.

Uwezekano wa kuwatenganisha upo asilimia ngapi?

Nini hasa chanzo cha issue hii ya yai la identical kushindwa kumalizia kazi ya kugawa viumbe kwa usawa? Mbegu ya kiume kushindwa kuitikia mwito wa yai? Au mbegu na yai vinatakiwa viwe designed kufanya kazi hiyo? Lakini inakuwaje viungo vingine vikamilike halafu vingine vinagoma?
 
Sasa kama moyo na ini wanategemeana watatenganishawaje?

Halafu eti vipimo vinaonesha kila mmoja ana mfumo wake wa damu. Natia shaka sana kama hili jambo litakuwa sawa kweli.
 
Hapa kwa asilimia kubwa kwa mujibu wa vipimo vya hao watoto hasa ku-share moyo na ini, hiyo operation ni sawa na assisted suicide. Halafu iweje daktari anasema mifumo yao ya damu haitegemeani halafu wana-share moyo?

Hapa lazima waalikwe mabingwa kutoka nje ya nchi pia na kuwepo na vifaa vya kutosha.
 
Back
Top Bottom