Watoto ni stress zinazotukumba wanaume wengi!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,031
Ngoja niende kwenye mada moja kwa moja!ni hivi katika swala la kulea mtoto wako hasa inapotokea mliachana na mama wa mtoto kwa namna moja au nyingine ni changamoto kubwa sana!hasa masingle mother walio wengi wanakuwa na ile hali ya kumkomoa baba wa mtoto kwa namna moja ama nyingine!mfano unaweza ukawa unamuhudumia mtoto kwa kutoa pesa za matumizi lakini pesa haziendi kwenye matumizi husika zaidi ya mwanamke kula good time mjini na hali ya mtoto kuonekana duni kama baba yake hajiwezi,pili either pesa za matumizi ya mtoto anaenda kununuliwa nguo mwanaume suruali flani hivi ili na yeye aonekana amepata handsame zaidi yako!na hali hii huchochea hasira kwa baba wa watoto wengi na kujikuta amesusa hadi kutoa matumizi yenyewe!Tatu pia imekuwa na swala la kawaida kwa masingle mother kutotaka baba wa mtoto asimuone mtoto wake ili mradi tu amkomoe!na kitu kingine asilimia kubwa ya wanawake (single mother)ndio wanaongoza kwa kujaza sumu watoto kwa kumdanganya mtoto mabaya ya baba yake!kuna kipindi wanaenda mbali zaidi hadi kudiriki kwa kumwambia mtoto baba yake amekufa!
N;B,Wanawake tofautisheni kati ya mapenzi na future ya mtoto!mtapata tabu saaana
 
Ni kutoa matunzo tu mwanzo mwisho hadi watakapokuwa na uwezo wa kujitegemea wao wenyewe kakiyamama!
 
Jaribu kuandika habari kwa kutenganisha Aya sio imeshikana kama Gauni.

Mbali na hilo, kama umegundua mama wa mtoto wako hana akili ipasavyo unaweza kununua baadhi ya mahitaji muhimu na kupeleka au kumtumia mtu wa karibu nawe ili awe anafikisha huduma kwa mwanao.
 
Jaribu kuandika habari kwa kutenganisha Aya sio imeshikana kama Gauni.

Mbali na hilo, kama umegundua mama wa mtoto wako hana akili ipasavyo unaweza kununua baadhi ya mahitaji muhimu na kupeleka au kumtumia mtu wa karibu nawe ili awe anafikisha huduma kwa mwanao.
Mkuu tumezoea kuunganisha kwenye mambo yetu hata huku tunaungalisha tu
 
Na unaanzaje kuzaa na mwanamke asiajali future ya mtoto wake...sawa imetokea kua ndio aina ya mwanamke aliekuzalia mtoto yuko ivyo. Hakikisha wanunua vitu muhimu kwa ajili ya mwanao ili hiyo kero ya mzazi mwenzio isikukumbe

Kama mtoto anasoma nenda kalipe ada mwenyewe huyo mwanamke mpatie risiti tu...mbona simple tu
 
Achaneni na kuzaa mtoto na mwanamke pasua kichwa.
Unaweza tamani ufe tu akose wa kumsumbua.

Unaweza piga bajeti ya mahitaji yote ya mwezi mzima na kumpa mama wa mtoto.
Baada ya wiki anakuambia "mwanao analala njaa huku"

Ukimfikiria mwanao unamuonea huruma.
Dawa unanunua
Mahindi gunia
Mchele debe mbili
Maharage nusu debe
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Sukari
Mkaa gunia
Unatuma mtu ampelekee.

Nguo na viatu navyo unanunua mwenyewe. Ni shida Sana haya maisha. Ukifikiria kumleta huku kwingine atateseka, kumuacha na mama yake unapata tabu Sana!!
Kama Bibi yake yupo hai na mtoto mkubwa mpelekee tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom