Kweli kabisa kakondoo. Inaboa kweli kuona watoto wakipata manyanyaso ambayo hawakustahili kabisa kupata huku wazazi wao wenyewe wakiangalia tu kama vile wako kwenye cinema.Asante sana mama mchungaji kwa hili jambo la msingi. Huwa nachukia kuona watoto wananyanyaswa na wazazi wa kambo huku wahusika wanakumbatia wenzi wao wapya na hata wakiambiwa hawajali, wakijidai kujali saana basi ujue watoto wataambulia kufokewa tu!! Sio fair!!!
Hee...kumbe Lizzy ni mama mchungaji? Bwana asifisiwe mama mch. Asante kwa darasa hili ntazingatia na kuchukua hatua nitakapolazimika kufanya hivyo.
Hili ni darasa tosha kwa kuwatunza watoto na kutaka kuanzisha mahusiano mpya.Kwa waliopo ndani. . . ..
7. Wafundishe watoto wako kumheshimu mwenzi wako ili kusiwe na matatizo kati yao.
Kwa ambao bado wako nje. . .
3. Usimtambulishe kwao mpaka utakapokua na uhakika kwamba urafiki/mahusiano yenu yana malengo. . . hii inasaidia kutowachanganya kwa kuwaletea wajomba/shangazi wapya kila siku.
4. Kabla ya kukubali muwe na mahusiano hakikisha anawapenda (LIKE, FOND OF, ADMIRE) watoto wako nao wanampenda yeye. Kama sivyo hali ilivyo usijidanganye kwamba mambo yatabadilika baadae. Hii itasaidia kukwepa ugomvi ambao utakua unakulazimu kuchagua upande kila wakati.
Kweli kbs Lizzy nimependa hii ilmu uliyotoa,kwan km watu tutakua makin na kuona umuhimu wa watoto/mtoto na uhusiano ukafuata hata tatizo la watoto wanaokimbia unyanywaji huko majumban na kuwa wa mitaan litapungua,ubarikiwe sn!
Hili ni darasa tosha kwa kuwatunza watoto na kutaka kuanzisha mahusiano mpya.
Hizo points nilizozibakisha ni muhimu sana kuzizingatia kabla ya kuanzisha mahusiano mapya hasa ikiwa watoto tayari wana uelewa, walikulia na kumuona mama/baba katika familia yao. Sasa unapofika wakati ikawa wazazi waliachana (au mmoja kutangulia mbele ya haki), watoto huwa si rahisi kumkubali mama/baba wa kuja kwa hofu hiyo ya kuwa amekuja kuchukua nafasi ya yule waliyempoteza.
Kwa hivyo, kabla ya kuanza upya, zungumza nao mpaka wakuelewe na upate ridhaa yao, na sio uanze kuwataka wamheshimu tayari yumo ndani. Kamwe usiwalazimishe kumkubali bali uende nao kidogo kidogo. Kadri wanavyokua ndivyo wanavyokuwa na uelewa zaidi wa mambo, sio wamempoteza mpenzi mama/baba yao baada ya mwaka moja au miwili unawaletea mtu mbadala.
Lizzy asante nimeipenda sana hii,imenipa extra knowledge and dimensions kwenye mapambano yangu ya maisha na kutoa experinece kwa wengi tu ambao labda muda bado au hayatakuja kuwapata lakini atleast they got some ideas when and only when it happens,thanks again.
Lakini hebu tupe extras, a freshly broken home,like that one.........utawaambiaje watoto below 12yrs old, kwamba mama/baba yuko wapi na kwa nini hayupo nyumbani.
Otherwise thanks again for your educative thread
CandidScope thanks for the article, that just shows how messed up some people are. Kuwaletea watoto wako baba anaefanana na huyo ni kuwaletea matatizo. Ila nadhani matendo ya hao wa kwenye article yako yanatokana na kukosa ule uhusiano wa baba na mwana, hivyo wanaona ni sawa kuwa wapenzi.
Malezi katika familia kwa watoto nayo yanatakiwa wazazi kuwa na uelewa mpana, ingawa watoto wanajua nini kinachoendelea kati ya wazazi, lakini si bora kuweka mambo hadharani kwani yanaweza kuathiri watoto. Uzungu nao tusipoangalia mambo gani ni ya kuiga yanaharibu watoto, ndio maana wazungu wengi wangali wadogo wanataka maisha ya bf/gf maana wanaona wanachofanya wazazi na hivyo wazazi hawawezi wazuia kwa vile dhamiri zinawasuta. Hivyo wazazi wanahalalisha watoto wadogo ambao hawajakomaa na kujua nini maana ya mapenzi kutumbukia kwenye ulimwengu huo wakati akili zao bado hazijakomaa na kuwa na utambuzi mkubwa.