Watoaji Wa "Matamko" Toenin na hapa

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,713
12,063
[h=3]KITENDO TULICHOKILAANI KUTENDEWA MKUU WA WILAYA IGUNGA CHAJIRUDIA TENA, NANI WA KULAUMIWA.[/h]
Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.

Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.

Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?

Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.

KAPINGAZ Blog haifungamani na chama chochote cha kisiasa, Tungependa kuwasikia TAMWA, TGNP na Taasisi nyingine za kijinsia mkikemea na kuvilaani vitendo hivi. Tulitegemea kitendo kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya kinaweza kikawa funzo pia kwa askari wetu lakini tunaona bado kinarudiwa tena.

Kwa hisani ya KAPINGAZ

Icheki apa dk 2:30 ,,,
Igunga Igunga ya Rostam yarejea kwa CCM - YouTube

Kwa hisani ya,,, HABARI NI HABARI NDUGU YANGU
 
raia huna haki hata aje nani kwa bongo ndivyo ilivyo mungu tunusuru na hili..amina!
 
Watoa matamko wamechoka kukurupuka. Maana kila mara watolea matamko mambo ambayo hawana uhakika nayo au kwa jazba tu mwisho wao wanaumbuka. Waache waendelea kumalizia tende za marehemu Ghadafi
 
Wacha tu wa2dharirishie dada na mama ze2 kwa kudai na kuzicmamia haki ze2 lakini nawaambia asubuhi haiko mbali kwa jina la ....hawa ma kinu watatafuta pakujificha .
 
Bakwata na wanazuoni wakiislamu mpo wapi?
Kwani ni mwislamu?angekuwa mwislamu ungewaona mapovu yanavyowatoka.Umesahau yule mbunge wa tabora Sakaya alivyodhalilishwa kwa kuwekwa mahabusu moja na wanaume, uliwasikia wakiongea chochote?Sababu anajina la kikristo hawahusu....!
 
Bakwata na wanazuoni wakiislamu mpo wapi?

Bakwata na Wanazuoni tupo, Ila tunasubiri CCM na akina Mukama watuandalie Tamko la kwenda kutoa kwa waandishi wa habari. Pia watupatie na jina lake na la mume wake tusije kuchemka tena kwa Fatuma Joseph Kimario yule DC wetu.
 
Haki ipo kwa public icons pekee, raia wa kawaida mara nyingi hutendewa vibaya sana na mambo kuisha kimya.

KITENDO TULICHOKILAANI KUTENDEWA MKUU WA WILAYA IGUNGA CHAJIRUDIA TENA, NANI WA KULAUMIWA.

Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.

Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.

Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?

Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.

KAPINGAZ Blog haifungamani na chama chochote cha kisiasa, Tungependa kuwasikia TAMWA, TGNP na Taasisi nyingine za kijinsia mkikemea na kuvilaani vitendo hivi. Tulitegemea kitendo kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya kinaweza kikawa funzo pia kwa askari wetu lakini tunaona bado kinarudiwa tena.

Kwa hisani ya KAPINGAZ

Icheki apa dk 2:30 ,,,
Igunga Igunga ya Rostam yarejea kwa CCM - YouTube

Kwa hisani ya,,, HABARI NI HABARI NDUGU YANGU
 
Wanagu wapendwa, mmeteswa na kukataliwa, mmetengwa na kudharauliwa, lakini nawaambia ipo siku haya yote yatapita!
 
Hata mimi nashangaa mpaka sasa hakuna tamko lolote lililotolewa..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom