Watetea haki za binadamu wako wapi?

Watetea haki za binadamu wako wapi?

hakuna watetea haki, bali watetea maslahi ya cdm na wenzao.
Iweje mtetea haki atetee madaktari kugoma wakati anajua watu wanakufa?
 
Taasisi za kiraiya za haki za binadamu za hapa nchini zina tetea watu kwa ubaguzi angalia kuawa kwa kamanda polisi mwanza zipo kimya. kukojolewa msahafu waislamu zipo kimya. kuawa polisui zanzibar wao kimya.wana mtetea ulimboka,mwangosi na mbowe.hii sio haki teteeni watu wote angalieni nchi za wezetu.

Issue ya kukojolea msahafu haihitaji wanaharakati kuachakazi zao nzito na kushughulikia upumbavu, naiitwa upumbavu kwasababu huwezi ku-create national attention kwa mabishano ya watoto. Tuna mambo mengi mazito yenye kulenga mustakabali wa taifa kama mgawanyo wa raslimali za taifa, ufisadi, matumizi mabaya yamadaraka na vingine vingi si huu ujinga wa wa ponda. Hii ni sawa na watu wenye magari kugombana eti sababu watoto wanaocheza waliona magari mawili yanapita na kuanza kubishana eti lilemoja ni bovu na jingine ni jipya. Kikwete alishawaambia kwamba zakuambiwa changanya nazako!
 
Huo ndio ubaya mbegu ya udini katika jamii. Ni vita mbaya kuliko ya kisiasa.
Hao wanaharakati tunaotaka watoe matamko tukumbuke ni wanazi au waumini wa dini mojawapo. Katika ofisi moja iwe ya chama cha siasa kama chadema au ccm hata hao wanaharakati kila mtu ni muumini wa dini mojawapo wa zinazobishana wakati huu. Na kila mmoja atakuwa na mtizamo au maoni yake kuhusu kinachoendelea. Sasa nani atoe tamko la taasisi wakati wanaotakiwa kutoa tamko hilo wengine ni wakristo na wengine ni waislamu?
Nafikiri kakaa kimya imekuwa ndio option sahihi ya kuonesha nutrality ya taasisi hizi kwenye malumbano yanayohusu dini. Tusilaumu tu tufikirie kwanza.

Hata hivyo ukweli utabaki 1+1=2 na sio 11
 
Sidhani kama ni sahihi kwa taasisi za kiraia (civil society) kujiingiza kwenye huu mgogoro wa kidini, at least not now.
 
Back
Top Bottom