Watengenezaji maudhui mitandaoni wamedai kuwa mifumo ya malipo nchini sio rafiki kwa wao kuweza kupokea fedha kutoka taasisi au makampuni mbalimbali ya mitandaoni, hali ambayo imekuwa pia kikwazo cha wao kuwa na uwanja mpana wa kunufaika na fursa hizo za mitandaoni.
Wakizungumza na Jambo TV Jijini Mwanza mara baada ya kufunga mafunzo ya watengenezaji maudhui ya mtandaoni, wameiomba Serikali kuangalia namna ya kufanya mazungumzo na makampuni au taasisi mbalimbali za mitandaoni kama Meta, Google na YouTube ili kunufaika na fursa.
Mtengenezaji maudhui ya mitandaoni kutoka Jijini Mwanza, Binagi George amesema mbali na hilo pia maudhui ya Tanzania yanalipwa kiwango kidogo cha fedha ukilinganisha na mataifa mengine kama Kenya na watengenezaji maudhui ya kiingereza.
"Sisi watengenezaji maudhui ya Tanzania kuna changamoto ambayo tunakutana nayo, ukiangalia platform mbalimbali za Tanzania tunapofanya hizi kazi namna ambavyo tunalipwa na hii mitandao ya kijamii ni tofauti kabisa na mataifa mengine mfano Kenya, sisi maudhui yetu yanalipwa kwa kiwango cha chini sana kwahiyo tunatamani kuona Serikali pia inatusaidia katika eneo hili," amesema Binagi.
Akizungumza mara baada ya kufunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ameomba masharti magumu ya utoaji mikopo kwa wasanii na watengenezaji maudhui yalegezwe ili kuwafikia vijana wengi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba akizungumza mafunzo hayo ambayo yamehudhurirwa na washiriki 274, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watengenezaji wa maudhui kufahamu nidhamu ya fedha pamoja na kubadilisha vipaji vyao kuwa chanzo cha kipato.
Pia soma: Makonda: Rais Samia ametoa Tsh. 2 Bilioni kwa ajili ya Watengeneza maudhui Mtandaoni (Content Creators)