Watendaji wa serikali Bukoba(M) ni tatizo sugu

Watendaji wa serikali Bukoba(M) ni tatizo sugu

Yametimia sasa na afadhari limetokea lililo nyeti zaidi ya niliyoyasemea hapa miezi miwili imepita. Wakati naandika haya bado kampuni ya hovyo ya MCL ilikuwa bado iko site wakiendelea na ujenzi wa miradi ya barabara hapa mkoani/manispaa na leo jamaa washamwaga manyanga na wamesepa na kijiji cha pesa

Mkataba wao ulikuwa ni wa zaidi ya 7bn ikiwa ni pesa kutoka WB baada ya zile za mara ya kwanza 18bn kukwamishwa na migogoro ya viongozi wa kisiasa wakati ule. Mwaka huu WB wakakubali wakaona isiwe taabu, wameingia mfukoni wakaanza kurudisha 7bn kwanza.

Sasa hii kampuni inasemekana ndiyo ile ile ambayo ilichanwachanwa na mh. rais akiwa ziarani Simiyu kwamba ni kampuni iliyokuwa na malori mawili tu huku ikiwa na miaka 5 mradi haujaisha. Wanasema ndo hiyo hiyo iliyokuja kupewa tenda hapa Bukoba, na leo mambo yao yale yale wameshindwa kazi.

Ajabu ni kwamba, hizi tenda zinatolewa chini ya wataalamu washauri wa manispaa wakiongozwa na injinia mkuu wa serikali kama msimamizi wa kazi za ujenzi. Na ikumbukwe ni mwaka huu huu mradi mwingine mkubwa wa ujenzi wa stand mpya umesimamishwa na DC baada ya mradi kujengwa chini ya viwango. DC alilamika sana na kumkemea sana injinia kwa kuendekeza ubabaishaji katika kazi na kupelekea miradi kujengwa chini ya viwango.

Hawa watendaji wa Kagera jamani ni vituko, ni miungu watu na ni wapigaji tu. Tumesema sana na tunasema tena wakubwa mtusikie, watendaji wenu huku ni bora kufuga mbuzi tukanywa supu na si hawa jamaa ...pesa za kodi zinafujwa huku
 
Afisa masoko na biashara tukutane hapa wiki hii kwa yanayokuhusu
 
Hakuna kitu kinaitwa Raisi wacha kudanganya watu
Idara zifuatazo hawajirekebishi na hawajifunzi,
1 Mazingira
2. Mipango miji
3 Ujenzi
4 Mipango na Uchumi

Ni idara ambazo kulindana kumezidi huku wananchi wakila shida za uhakika. Sisi wananchi tumemwelewa sana raisi wetu na tutamsaidia kwa kila hari. Kulindana kwenu na kujuana kunatakiwa kukoma mara moja ama sivyo tutawashitaki wazi wazi kwa mwajiri wenu mkuu mh. JPM

Tend a zenu, mipango miji yenu, usafi mjini, ujenzi wenu, kusuasua kurasimisha njia za mapato na mihanya inayoachwa makusudi ili watu fulani fulani wale yanatakiwa kukoma. Hii ni rai yetu kwenu, badilikeni mapema
 
Wale wa mipango mji kwa nini Mji wa Bukoba munaruhusu wafungwa -magereza kukata miti mji mzima Je munataka mji wetu wenye madhali nzuri ugeuke jangwa? Wale viongozi waliofanya campaign ya kupanda miti mji mzima munafikiri hawakufanya jambo jema.Nenda Moshi ,Arusha si mazingira ya miji yao yanapendeza.Tunaomba viongozi wa mji wetu wa BUKOBA kuiga mfano mzuri waimize watu wapande miti mizuri ya vivuri na watunze mazingira.BADO tunawakumbuka VIONGOZI WALIOPITA KAMA CHANGA,MASAWE Kwa jitahada zao za kuhimiza usafi,na kupanda miti.Kata mti panda mti usikate miti ambayo hukuipanda
 
Idara zifuatazo hawajirekebishi na hawajifunzi,
1 Mazingira
2. Mipango miji
3 Ujenzi
4 Mipango na Uchumi

Ni idara ambazo kulindana kumezidi huku wananchi wakila shida za uhakika. Sisi wananchi tumemwelewa sana raisi wetu na tutamsaidia kwa kila hari. Kulindana kwenu na kujuana kunatakiwa kukoma mara moja ama sivyo tutawashitaki wazi wazi kwa mwajiri wenu mkuu mh. JPM

Tend a zenu, mipango miji yenu, usafi mjini, ujenzi wenu, kusuasua kurasimisha njia za mapato na mihanya inayoachwa makusudi ili watu fulani fulani wale yanatakiwa kukoma. Hii ni rai yetu kwenu, badilikeni mapema
Watendaji wengi wa serikali kwa ujumla ni mwiba mchungu kwa serikali ya Rais Magufuli.Kunahitajika Marshall Plan ya
ku-over haul utumishi wa umma,vinginevyo juhudi zote za Rais Magufuli zitakuwa bure.Kuondoa watu wenye vyeti fake is a cosmetic overture,and only a first step in reforming the public service,but is not in any way enough.Tatizo ni kubwa zaidi ya vyeti fake.
 
Ndugu yangu Chibolo nazingua wapi mkuu ili niweze kukuelewa sawia
 
Asante sana mh. Mabura kwa kunishika mkono juu ya hawa wasanii wanajiita wakuu wa Idara. Idara za manispaa nyingi ni za kibabaishaji na ni wezi, wavivu na miungu watu
Bukoba manispaa ni mzigo mkubwa sana
 
Back
Top Bottom