Watendaji wa Kata Manispaa ya Tabora wasitisha ushirikiano na Mkuu wao wa Wilaya DC Komany Kitwala.

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Katika hali ya kushangaza Mkuu wa wilaya ya Tabora Mh.Komanya Kitwala ,aliwaita watendaji wa kata za Manispaa ya Tabora ofisini kwake,baada ya watendaji kufika ili kusikiliza walichoitiwa.

Jambo la kushangaza DC kitwala aliwaamuru watendaji kupiga magoti sakafuni.


Watendaji wawili walipiga magoti huku waliosalia wakimgomea kupiga magoti kwa madai kuwa hawana kosa na kuwa adhabu ya magoti ni udhalilushaji.

Baada ya kugoma hata wale walliopiga magoti nao wakanyanyuka na kuungana na wenzao.

DC akapiga simu kwa OCD ili wakatupwe ndani.

Walichukuliwa na polisi hadi kituo cha kati.

Hata hivyo OCD kwa busara zake hakuwaweka ndani baada ya kuwasilikiliza.

Aliwaruhusu waondoke kwenda kuendelea na kazi mpaka atakapowaita .

Watendaji wameandika Barua kwenda Ofisi ya Rais Tamisemi kwa lengo la kutoa malalamiko yao dhidi ya Mkuu wao wa Wilaya.

Ni imani ya wengi kuwa huu utakuwa mwisho wa huyu DC anaejiona mungu mtu ndani ya Manispaa ya Tabora.

Mamlaka za uteuzi zinamfahamu vizuri sana huyu DC,malalamiko ni mengi kutoka kila upande dhidi ya tabia mbaya za huyu DC.
Kagombana na katibu wa CCM wa Wilaya.

Kagombana sana na Mkurugenzi

Kila dereva yeye hamtaki

Watumishi wa umma wananyanyaswa na huyu DC.
Aligombana na katibu Tarafa,mpaka sasa katibu tarafa akahamisha Ofisi toka pale kwa DCna kuhamia mtaani ili kujiondoa kwenye migogoro isiyoisha.

Mpaka muda huu Watendaji wameazimia kuto toa ushirikiano wowote kwa huyu DC.

Hayo ndiyo yanayoendelea Tabora.
 
Kama ni Watendaji wa Kata acha awakomeshe. Hawa jamaa ndio walishirikiana bega kwa bega na Jiwe pamoja na MaCCM kufanya kila aina ya dhuruma dhidi ya upinzani.

Tena ningetamani hata angewatandika bakora kabisa.
 
Watendeji Ni wapumbavu wacha awakomeshe. Waliharibu uchaguzi wasione maumivu Yao tu Kuna maumivu wamefanya zaidi ya wanaopata wao. Jinga kabisa hao
 
Makada wote hao,watapatana tu.
Wametuchelewesha sana,uongo ndugu zangu,ndiooooooo!
 
Back
Top Bottom