Watendaji serikalini wameoza

Watendaji serikalini wameoza

Noor

Senior Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
146
Reaction score
49
Ndg zangu. Kila siku zinalaumiwa baadhi ya wizara, hasa ya Elimu, Mambo ya ndani na nyingine kadha wa kadha. Ila swali langu je ni wizara au idara ipi iliyo makini kama zote si sawa kwa utendaji wenye udhaifu mkubwa?

Karibia wizara zote nilizowahi tembelea kazi ya kufanyika dakika 5 wao wanaifanya siku mbili. Rushwa imeota mizizi kwa watendaji wa wizara ili jambo lako lishughurikiwe haraka.
 
[QUOTE=Pole sana.ufanisi wa kazi Tz una kasoro nyingi usiojaa tija.Mtu anakuja ofisini kuchezea komputa na karata.Kwa mfumo huo kazi haiwezi kuwa na ufanisi kwa sababu baada ya saa za kazi hakuna msimamizi wa ofsi anauliza ukubwa wa kazi uliofanyika siku hiyo .Ufanye usifanye yote sawa.Serikali inashindwa na mwenye baa maana kila siku anauliza umeuza chupa ngapi.mshahara kwa chupa.
 
Ndg zangu. Kila siku zinalaumiwa baadhi ya wizara, hasa ya Elimu, Mambo ya ndani na nyingine kadha wa kadha. Ila swali langu je ni wizara au idara ipi iliyo makini kama zote si sawa kwa utendaji wenye udhaifu mkubwa?

Karibia wizara zote nilizowahi tembelea kazi ya kufanyika dakika 5 wao wanaifanya siku mbili. Rushwa imeota mizizi kwa watendaji wa wizara ili jambo lako lishughurikiwe haraka.
Katika serikali kuna kitu kinaitwa Government Bureaucracy; unajua dokezo sabili wewe, unajua dokezo wewe, unajua minute ladder, unajua minute sheet? Unajua masjala ya wazi ama masjala ya siri? Mkuu tatizo ni kwamba kila kitu serikalini lazima kifuate utaratibu fulani/mlolongo fulani. Hata kama watu wanafanya kazi unaweza kuambiwa uje kesho kwa sababu ya utaratibu! Hii si kwamba napinga kuwepo kwa masuala ya rushwa kwa sababu hayo yapo kwenye public domain lakini pia hii ya majalada lukuki iangaliwe. Government haijawa automated. Nasikia imeanzishwa eGovernment Agency huenda hii ikasaidia kuexpediate automation ya serikali.
 
Mkuu kama kazi yako walifanya siku 2 basi wewe una bahati sana.

Kwa kawaida kazi ya dk 5 wao huifanya kuanzia mwezi mmoja na kuendelea.

Pale wizara ya Ardhi town ndio wanaboa kabisa unaenda leo unaambiwa njoo mtondogoo , ukija hiyo mtondogoo unamkuta yule yule uliyemkuta majuzi aliyekwambia uje tena ndio kwanza anakushangaa anakuuliza nani alikwambia uje leo? Unamsuta unamwambia ni wewe mwenyewe tena ulikuwa umevaa shati la pinki ulisimama paleee! anaanza kuona noma anakwambia hiyo kazi bado njoo baada ya wiki 2. Ukija baada ya wiki 2 unamkuta mtu mwengine nae anakushangaa anakwambia hana taarifa za ufuatiliaji wa hilo swala labda ujaze fomu upya.

Hapo mtu mzima umetokea Bunju B umepanda mabasi sijui mangapi ya kuungaunga kufika pale, na foleni barabarani.

Watumishi wa serikalini ni $%^&!!!!!!
 
Utaratibu si tumeiweka wenyewe? kwanini tusiubadilishe au kuondoa?

Dawa ya serikalini ni kuwa na ajira za muda mfupi mfupi kila miaka 3 unatangaza tena watu wanaomba maana nguvu kazi ipo kibao haina kazi.
 
Mkuu ni kweli tumeweka wenyewe lakini ndio maana nikasema inabidi iwe automated ila hiyo automation ndio inaenda kwa mwenda wa bureaucratic race.

Mkuu kuna watu walijaribu kuweka ajira za muda mfupi lakini wakakutana na kichaka kinaitwa Permanent and Pensionable.
 
Mkuu kama kazi yako walifanya siku 2 basi wewe una bahati sana.

Kwa kawaida kazi ya dk 5 wao huifanya kuanzia mwezi mmoja na kuendelea.

Pale wizara ya Ardhi town ndio wanaboa kabisa unaenda leo unaambiwa njoo mtondogoo , ukija hiyo mtondogoo unamkuta yule yule uliyemkuta majuzi aliyekwambia uje tena ndio kwanza anakushangaa anakuuliza nani alikwambia uje leo? Unamsuta unamwambia ni wewe mwenyewe tena ulikuwa umevaa shati la pinki ulisimama paleee! anaanza kuona noma anakwambia hiyo kazi bado njoo baada ya wiki 2. Ukija baada ya wiki 2 unamkuta mtu mwengine nae anakushangaa anakwambia hana taarifa za ufuatiliaji wa hilo swala labda ujaze fomu upya.

Hapo mtu mzima umetokea Bunju B umepanda mabasi sijui mangapi ya kuungaunga kufika pale, na foleni barabarani.

Watumishi wa serikalini ni $%^&!!!!!!
Kila kitu mwisho wake lazima afanye raisi ambaye naye IKULU hakukaliki duh nchi imeanguka,kuinua tunahitajika wote lazima tuamue sasa
 
Kuna umuhimu wa wananchi kuamaka na kusema no kwa hii serikali, ili ijirekebishe maana ni usumbufu kwa wananchi hasa wakipato cha chini wale wenye pesa zao wananyenyekewa na mambo yao kwenda faster. RAIA WAKAWAIDA UKITAKA KULASIMISHA KITU CHAKO NI USUMBUFU KUFA, ACHA FISADI AOPITE KILA MFANYAKAZI MBILI HAIKAI TATU HAIKAI KUMSUJUDIA HUYO MTU WATAKIMBIZA FAILI HADI LISHUGHULIKIWE DAKIKA TANO, NA TARATIBU ZOTE LITAPITIA.
 
Haitatokea kamwe kwa serikali ya magamba kufanya kazi kwa wakati na mpangalio ulio mzuri hadi hapo tutakapoamua kufanya mabadiliko. Nasema hivi kwasababu siasa ipo mpaka kwenye utendaji wa kazi za kila siku za serikali haijali ni ofisi gani unakwnda kupata huduma.
 
Katika serikali kuna kitu kinaitwa Government Bureaucracy; unajua dokezo sabili wewe, unajua dokezo wewe, unajua minute ladder, unajua minute sheet? Unajua masjala ya wazi ama masjala ya siri? Mkuu tatizo ni kwamba kila kitu serikalini lazima kifuate utaratibu fulani/mlolongo fulani. Hata kama watu wanafanya kazi unaweza kuambiwa uje kesho kwa sababu ya utaratibu! Hii si kwamba napinga kuwepo kwa masuala ya rushwa kwa sababu hayo yapo kwenye public domain lakini pia hii ya majalada lukuki iangaliwe. Government haijawa automated. Nasikia imeanzishwa eGovernment Agency huenda hii ikasaidia kuexpediate automation ya serikali.

Hiyo nimeipenda mkuu,Hata hizo Agency ni fake ndiyo miradi ya wizara kuchukua pesa kirahisi serikalini. Tuna kazi kubwa sana ili nchi hii iendelee. Ukitaka kujua adha ya kufuatilia vitu serikalini waulize wastaafu wanavyopata taabu.Hayo madokezo ni ya safari tu hakuna kazi mkuu tunahitaji ukombozi wa fikra wa viongozi wetu siyo wa Agency. Hayo mambo ya permanent and pensionable ndiyo yanaongeza uzembe serikalini, watu wanashikilia nafasi kwa hirizi siyo kwa sifa.Tunatakiwa kuleta mabadiliko ya kweli kwa kufanya maamuzi magumu.
 
Ofisi za Serikali zina matatizo mengi. Lakini tatizo kubwa ni kutojua wajibu wao. Amini usiamini Watumishi wengi wa umma hawajui au wamejisahaulisha wajibu wao wa kuwatumikia wananchi. Badala yake wanajiona wako juu ya wananchi wa kawaida. Ndo maana mtu haoni shida wala aibu kumwambia mteja njoo siku flani kila siku.

Kimsingi kunahitajika mageuzi makubwa katika utumishi wa umma. Bahati mbaya wizara inayoshughulikia mambo ya utumishi wa umma inaonekana wizara ya kustarehe hawaumizi kichwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabilu public service.

Wanakuja na vitu ambavyo havijibu au havitoi suluhisho. Mfano wametumia mabilioni ya fedha kuweka client service charters ambazo zimefungiwa makabatini. Wametumia mabilioni mengine kuweka mfumo wa opras ambao haufanyikazi.

Sheria za utumishi wa umma inabidi zibadilishwe. Tuwe na ajira za mikataba na wakurugenzi wapewe mamlaka ya watumishi walio chini yao. Na adhabu kali itolewe kwa wanaotumia madaraka vibaya.
 
Kimbunga hebu angalia mfano huu halisi ulionitokea,jiji walikuja ktk maeneo yetu kupima mwaka 2010,wakasema watatupa fidia kwa ajili ya mradi,ilikuwa october wakasema after six months watakuwa wamemaliza zoezi lote la kulipa fidia.
Huu ni mwaka wa 2013 mara ya mwisho tuliitwa august 2012 na mkuu wa wilaya,akasema kwa unyenyekevu zoezi limemalizika,pesa zipo imebaki mkuu wa mkoa tu kusign cheki.kwa hiyo akaahidi witin 3 weeks zoezi litakuwa limeisha,..guess what she was a lier mpaka 2013 march kimya,
ni nini hii?
Toeni kitengo cha ardhi mu outsource kwa makampuni private kwa ajili ya upimaji coz kama mmeajili mtu kwa ajili ya kupima ila kila siku anaamkia ofisini na sio site what is it?

Mkuu ni kweli tumeweka wenyewe lakini ndio maana nikasema inabidi iwe automated ila hiyo automation ndio inaenda kwa mwenda wa bureaucratic race.

Mkuu kuna watu walijaribu kuweka ajira za muda mfupi lakini wakakutana na kichaka kinaitwa Permanent and Pensionable.
 
f
Hiyo nimeipenda mkuu,Hata hizo Agency ni fake ndiyo miradi ya wizara kuchukua pesa kirahisi serikalini. Tuna kazi kubwa sana ili nchi hii iendelee. Ukitaka kujua adha ya kufuatilia vitu serikalini waulize wastaafu wanavyopata taabu.Hayo madokezo ni ya safari tu hakuna kazi mkuu tunahitaji ukombozi wa fikra wa viongozi wetu siyo wa Agency. Hayo mambo ya permanent and pensionable ndiyo yanaongeza uzembe serikalini, watu wanashikilia nafasi kwa hirizi siyo kwa sifa.Tunatakiwa kuleta mabadiliko ya kweli kwa kufanya maamuzi magumu.

Umesema ukweli. Watumishi wanabweteka kwa sababu wana ajira ya kudumu. Anajua anopokosea anahamishwa tu, mshahara uko pale pale. aki underperform hakuna wa kumchukulia hatua. Hawa watu waajiriwe kwa mikataba na performance goals ziwekwe kwenye mkataba (opras) kwa miaka 5. asipo perform achukuliwe mwingine. Watanzania kibao wanauwezo na uzalendo wako mtaani
 
Ofisi za Serikali zina matatizo mengi. Lakini tatizo kubwa ni kutojua wajibu wao..

Wanajua sana wajibu wao ni makusudi tu wanafanya.

Kama mtumishi anatoka kwake asubuhi ameacha pesa ya mboga anaenda kugombania daladala hadi shati linachanika huyu kweli hajui anafuata nini posta kule?
 
Back
Top Bottom